Wadau wa Michezo washauriwa kuwekeza katika Viwanda.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa
Michezoalipokuwa akizindua uzinduzi wa Channeli mpya za Michezo kutoka
kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akijadiliana jambo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Fernandez wakati wa uzinduzi wa
Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikata utepe kuashiria uzindua
wa Channeli mbili za michezo ambazo ni TING Michezo HD 1 na TING
Michezo HD 2 kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Michezo la Taifa Bw.Said Kiganja akionesha zawadi ya King’amuzi
aliyopewa na Kampuni ya TING wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za
Michezo kutoka Kampuni hiyo Agosti 28,2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
TING Dkt .Veron Fernandez akielezea kuhusu faida za channeli mbili mpya
za michezo kutoka katika kampuni yake zitakavyosaidia kukuza Michezo
nchini Agosti 28,2016.
……………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi – WHUSM
Wadau wa Michezo nchini
wameshauriwa kujenga viwanda kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya michezo
ili kuleta maendeleo katika sekta hiyo.
Ushauri huo umetolewa jana na
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura alipokuwa akizindua channeli mbili za Michezo za Kampuni ya
king’amuzi cha TING.
Naibu Waziri Anastazia alisema
kuwa kwa kupitia uwekezaji huo kutasaidia kuinua sekta ya michezo nchini
pamoja na kuondokana na changa moto ya vifaa vya michezo jezi za
michezo,mipira na vifaa vinginevyo.
“Tuunge mkono juhudi za Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwekeza katika viwanda
vitakavyotengeneza vifaa vya michezo” alisema Mhe. Anastazia
Aidha, Naibu Waziri huyo aliongeza
kuwa kuwepo kwa viwanda hivyo kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa
vifaa vya michezo nchini kwani vifaa vingi vya vinatoka nje ya Tanzania
hivyo huuzwa kwa bei ya juu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya TING Dkt. Veron Frenandes ameishukuru Serikali
kwa kutoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wa Michezo nchini katika
kukuza na kuendeleza sekta hiyo.
Chaneli za Michezo zilizozinduliwa
katika Kingamuzi hicho ni ni TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2
ambazo zitakuwa zikionesha michezo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni