Kampeni ya kuwania kujishindia malori ya konyagi yazidi kushika kasi
Meneja Chapa wa Konyagi Martha Bangu akiongea na mawakala  katika hafla ya uzinduzi wa kampeni mkoani Arusha
Baadhi ya mawakala na wafanyakazi wa TDL wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni mjini Arusha
Maofisa wa TDL katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Arusha
…………………………………………………………………………..
Kampeni ya kuwania kujishindia 
malori ya usambazaji iliyolenga kuwanufaisha mawakala wa kampuni ya 
Tanzania Distilleries   kupitia kampeni inayojulikana kama 
“Nunua,Uza,Shinda na Konyagi inazidi kushika kasi kadri muda wake wa 
kumalizika unavyosogea ambapo mawakala wanaendelea kuchuana kuuza bidhaa
 za kampuni kwa ajili ya kufikia lengo lililowekwa ili waweze kushiriki 
kwenye droo ya kupata washindi itakayofanyika mapema mwezi Oktoba.
Kampeni hiyo ambayo imewalenga 
wasambazaji katika mikoa  yote nchini itawawezesha washindi  2 
kujishindia kila mmoja lori aina ya Eicher  yenye uzito wa tani 3 na 
pia  katika kipindi hiki cha kampeni wanaendelea kujipatia zawadi 
mbalimbali.
Akiongelea maendeleo ya kampeni 
hii baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi wake kwenye kanda za mikoa 
mbalimbali,Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe,alisema
 kuwa mwitikio wa mawakala katika kushiriki ni mzuri  kinachosubiriwa ni
 washindi wawili kujinyakulia malori ya kuwarahisishia  zoezi la 
usambazaji na biashara zao kwa ujumla.
“Natoa wito kwa mawakala wetu 
kuendelea kushiriki katika kampeni hii na kufikisha malengo ya kuingia 
kwenye droo kwa kuwa imeandaliwa kwa ajili yao kwa ajili ya kuwawezesha 
na tunachosubiri ni kuona magari haya yatachukuliwa na wasambazaji 
kutoka kanda gani.
Kavishe alisema lengo kubwa la 
kampeni hii ambayo imesifiwa na wasambazaji wa vinywaji vya kampuni hiyo
 kutokana na kuwa na zawadi kubwa ni kuwainua kibiashara wasambazaji wa 
bidhaa za kampuni ikiwemo kuwapatia motisha kutokana na kushirikiana na 
kampuni kibiashara.
“TBL Group tunazo Programu 
mbalimbali za kuwezesha wateja wetu na ndio maana tumekuwa tukiandaa 
promosheni mbalimbali zenye lengo la kuwainua kimaisha ikiwemo kuwapatia
 mafunzo mbalimbali ya mbinu za kufanya biashara kwa mafanikio”.Alisema
Alisema kampeni itadumu kwa 
kipindi cha wiki 12 na wasambazaji wanaoshiriki wamewekewa viwango vya 
mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa
 ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu . “Tunaamini kabisa kampeni 
hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya 
manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.
Baadhi ya mawakala wamepongeza 
jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa za promosheni ambazo 
zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya zawadi 
ndogondogo  zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.
Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya 
Konyagi kanda ya Kusini aliyejitambulisha kama Saimon Haule amesema kuwa
 japo sio mawakala wote watapata malori lakini watakaobahatika kushinda 
watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha biashara kukua. 
“Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo vya 
kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni