Tamasha la Uhondo wa Zantel lakonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
:Meneja Habari na Uhusiano wa 
kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia)  akitoa 
maelezo kwa  baadhi ya wakazi wa Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la  
Dares Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu huduma mpya zitolewazo na kampuni 
hiyo ikiwa ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya
 katika kuboresha bidhaa zake  na kutoa huduma bora kwa wateja. Ilikuwa 
ni katika tamasha lililopewa jina la Uhondo wa Zantel lililodhaminiwa na
 kampuni hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya 
anayetesa na wimbo wake maarufu wa ‘Unanitega Shemeji’, Selemani Jabil 
‘MsagaSumu’ akifanya vitu vyake wakati wa tamasha la ‘Uhondowa Zantel’ 
lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam mwishoni
 mwa wiki. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Zantel.
Meneja Habari na Uhusiano wa 
Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Winnes Lyaro (kulia)  akitoa 
zawadi kwa mmoja wa washindi wa maswali ya papo kwa papo wakati wa 
tamasha la ‘Uhondo wa Zantel’ lililofanyika Boko Basihaya nje kidogo ya 
Jiji la Dar es Salaam. Tamasha hilo lililodhaminiwa na Zantel kama 
sehemu ya mikakati ya kampuni hiyo inayokuja na mtizamo mpya katika 
kuboresha bidhaa zake na kutoa huduma bora kwa wateja.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni