MAKABIDHIANO YA OFISI MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA- NIDA
Dr. Modestus Kipilimba (Kushoto)
akimkabidhi ripoti ya utekelezaji mradi wa vitambulisho vya Taifa Bw.
Andrew Wilson Massawe aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA
wakati wa hafla ya Makabidhiano katika ofisi za Makao makuu ya NIDA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Bw.
Andrew Wilson Massawe akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa mara baada ya hafla ya makabidhiano
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba aliketi kushoto na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bw. Andrew Wilson Massawe wakiwa katika picha
ya pamoja na Menejimenti ya NIDA, baada ya hafla fupi ya makabidhiano
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Bw.
Andrew Wilson Massawe akikagua mitambo ya uzalishaji vitambulisho
alipotembea kituo cha uchakataji na uzalishaji vitambulisho mara baada
ya halfa ya makabidhiano. Kulia ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA
ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa akishuhudia
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA,
akikagua mfumo wa uhifadhi taarifa wakati alipotembelea kituo cha
uchakataji taarifa (Data Centre) na kushuhudia mfumo wa kielektroniki
unavyoendesha shughuli mbalimbali za uzalishaji na uhifadhi wa taarifa
katika kituo hicho
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu
NIDA ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dr.
Modestus Kipilimba akifafanua jambo wakati akihitimisha ziara ya
makabidhiano katika kituo cha uchakataji na uzalishaji vitambulisho.
Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Bw. Andrew Wilson Massawe akiwa
ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti
…………………………………………………………………………….
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa
Idara ya Usalama wa Taifa Dr. Modestus Kipilimba leo amekabidhi rasmi
ofisi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu mpya Bw. Andrew Wilson Massawe;
aliyeteuliwa hivi karibu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA
Katika Hafla fupi ya makabidhiano
iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, Dr.
Modestus Kipilimba amekabidhi ripoti yenye mjumuisho wa taarifa ya
utekelezaji mradi wa Vitambulisho vya Taifa na hatua za utekelezaji
Halfa hiyo ilifuatiwa na ziara
fupi ya kutembelea kituo cha uchakataji taarifa na uzalishaji
vitambulisho (Data Centre) ambapo mbali na kukagua shughuli za
uzalishaji, Bw. Massawe alipata fursa ya kukagua mitambo na ubora wa
vitambulisho vinavyozalishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni