MATUKIO MKUTANO WA WAFANYABIASHARA KIGOMA NA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO
Waziri
 wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa
 makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu, 
akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye 
ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka
 ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane 
ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao
Bi. 
Rehema Kabuye, (Katikati) ambaye ni mke wa Nahodha wa Meli ya Mv Liemba,
 inayotoa huduma zake Ziwa Tanganyika, akimwonesha Waziri wa Fedha na 
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), picha za mtoto wake ambaye ana 
matatizo ya kiafya, akimsihi Waziri huyo amsaidie yeye pamoja na wenzake
 ili waume zao walipwe mishahara yao ya miezi 8 wanayomdai mwajiri wao, 
Mamlaka ya Huduma za Meli mkoani Kigoma.
Katibu
 wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba (Kulia), akichukua maelezo
 ya kina kutoka kwa Bi. Rehema Kabuye, Mkazi wa Kigoma, ambaye amemwomba
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aingilie kati
 sakata la waume zao wanaofanya kazi kwenye mamlaka ya huduma za meli 
mkoani Kigoma, ambao hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu.
Baadhi
 ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa 
fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati 
wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na 
ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, 
mjini Kigoma.
Baadhi
 ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa 
fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano na 
Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi, 
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Baadhi
 ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini 
hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), 
wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, mkutano 
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri
 wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aliyesimama kushoto,
 akiwahutubia wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali 
ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa 
mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Katibu
 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Kigoma Bw. Raymond Ndabiyegetse 
(katikati) akichangia hoja katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango, 
Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) ambaye alipongeza juhudi 
zinazofanya na Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya biashara 
zao.
Mkurugenzi
 wa kampuni ya Aifola ya Mjini Kigoma, Bw. Zubery Mabie, akiongea kwa 
hisia kali akishutumu TRA na maafisa wengine wa serikali katika kituo 
kidogo  cha Forodha cha Manyovu kilichoko mpakani mwa Tanzania na 
Burundi, kujihusisha na rushwa kwa kupitisha maroli yakiwa na mizigo, 
ikiwemo chokaa anayozalisha, bila kulipia kodi. Mhe. Dkt. Philip Mpango 
(Mb), ameahidi kulifanyiakazi suala hilo.
Mmoja
 wa wafanyabiashara wa Mjini Kigoma akichangia hoja katika mkutano 
ulioitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb),
 kuhimiza ulipaji kodi, matumizi adili ya fedha za umma, matumizi ya 
Mashine za Kieletroniki na utoaji wa risiti,  mkutano uliofanyika katika
 ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Askofu
 Mstaafu wa Kanisa la Anglican, Dkt. Gerard Mpango, akitoa mchango wake 
wa mawazo ambapo ameitaka serikali kutoa elimu ya kutosha ya biashara na
 ujasiriamali kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kutumia fursa 
zilizopo katika soko la Afrika Mashariki, kukuza mitaji na biashara zao,
 wakati wa mkutano wa wafanyabiashara  na Waziri wa fedha na Mipango, 
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), hayupo pichani, uliofanyika katika ukumbi 
wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Kamisha
 Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia masuala ya
 kodi, Bw.  Shogholo Msangi akifafanua kuhusu kodi ya Ongezeko la 
Thamani (VAT) kwa wafanyabiashara wa Kigoma Mjini wakati wa  mkutano na 
 Waziri wa  Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (mb).
Waziri
 wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango (Mb), akizungumza na 
wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo 
umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya mashine za kieletroniki pamoja na 
kuwasisitizia kutoa risiti kwa wateja wao. kushoto kwake ni Kamishna 
Msaidizi anayeshughulikia masuala ya kodi, Wizara ya Fedha na Mipango, 
Shogholo Msangi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, 
mjini Kigoma.
Waziri
 wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionesha rundo la 
makaratasi yaliyoandikwa hoja na kero mbalimbali za wafanyabiashara wa 
mjini Kigoma, wakati wa mkutano kati yake na wafanyabiashara hao, 
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Waziri
 wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiwa 
katika picha ya pamoja na Askofu Dkt. Gerard Mpango, baada ya kumalizika
 kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mjini Kigoma, 
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
 
Waziri wa  Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) 
akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto 
Kabwe, wakati wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa NSSF, ulipofanyika 
mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa mjini 
Kigoma.
Mbunge
 wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe  (kushoto), akisisitiza jambo wakati 
akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Mpango (Mb), baada
 ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wafanyabiashara wa mjini Kigoma,
 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni