Jumatano, 3 Agosti 2016
Tanzania
inazidi kupiga hatua kila uchwao kwenye masuala mbalimbali hivi
karibuni ilishuhudiwa kwenye masuala ya Filamu mwanadada Elizabeth
Michael (Lulu) na Single Mtambalike wakileta ushindi nchini baada ya
kushinda tuzo za Filamu za African Magic Viewers Choice Awards 2016
zilizotolewa jijini Lagos, Nigeria., huku kwenye Tasnia ya Muziki
ikishuhudiwa msanii Alikiba akisaini Mkataba na kampuni kubwa ya Sony
ambapo kwa bara la Afrika yeye na msanii Davido wa Nigeria ndio wamepata
fursa hiyo adhimu.
Kwa
upande wa masuala ya Kiroho imeshuhudiwa kwa kijana Rajai Ayoub
kushinda katika mashindano ya usomaji wa Qur-an kwa mtindo wa Tajweed
yaliyo fanyika nchini Iran na kushika namba moja kwa kwa Afrika na namba
sita kwa Dunia, huku katika kipengele cha uzuri wa Sauti akichukua
namba moja kwa Dunia nzima.
Halikadhalika
katika nyanja za Maendeleo Tanzania imezidi kufanya vizuri ambapo
kijana Selemani Yusuph Kitenge amekuwa miongoni mwa vijana waliotunukiwa
tuzo za Diploma ya Heshima maarufu kama 'New Leaders For Tommorow
Diploma' zinazo tolewa na Taasisi ya Crans Montana Forum yenye makao
makuu yake nchini Monaco na Uswis.
Akizungumza
na Mtembezi.com Selemani Kitenge ameeleza kuwa moja ya sababu
zilizopelekea kutunukiwa tuzo hiyo ushiriki wake wa mijadala mbalimbali
ya masuala ya kimaendeleo katika nchi za Russia, Moroco na Azerbaijan,
ndipo wadau mbalimbali wakapendekeza jina lake katika tuzo hizo, kwa
Tanzania ni mara ya kwanza kwa kijana Selemani kutunukiwa tuzo hiyo
tangu zianzishwe mwaka 2010 ambapo atapata fursa ya kushiriki mikutano
mbalimbali ya kimataifa itakayo wahusisha viongozi wakubwa wa kidunia,
ambapo amewataka vijana kutokata tamaa na kuamini katika kile
wanachokifanya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni