PROF WANGWE ATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Prof Samwel Mwita Wangwe amesema
kuwa uongozi wa Awamu ya Tano umefanya kazi kubwa katika kuweka maslahi
ya Taifa mbele ikiwamo kuongezeka kwa bajeti ya maendeleo na kupunguza
matumizi ya serikali.
Hatua hii imesaidia nchi kusonga
mbele kupitia uboreshaji wa utendaji kwa watumishi wa umma na hivyo
kujenga imani kubwa kwa wananchi juu ya Serikali yao.
Profesa Wangwe ametoa kauli hiyo leo mjini Dar es salaam wakati akitoa tathmini ya uongozi wa Awamu ya Tano.
Amesema kuwa Rais Magufuli katika
uongozi wake umesaidia kuokoa fedha nyingi za walipa kodi ambazo
zilikuwa zikiishia mikononi mwa watu wachache na kuzielekeza katika
shughuli nyingine za maendeleo.
Profesa Wangwe amewataka wananachi
kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye harakati zake za kupambana na
matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwa matokeo yake yatasaidia
kuijenga Tanzania mpya ambayo kila mwananchi atapata fursa kunufaika na
rasilimali za nchi.
“Kwa kweli Rais huyu amefanya
mabadiliko makubwa sana na kwa sasa nchi imerudi katika hali nzuri,
kwani nchi ilikuwa imefika mahali pabaya na kwa hiyo aliona ni budi
kuhakikisha Rushwa na Ufisadi vinakomeshwa na kwa hili ameanza vizuri na
nchi inakwenda katika mwongozo mzuri kwani ameboresha utendaji kazini
serikalini na kubana matumizi ambayo yamesaidia kuokoa pesa nyingi
ambayo inatumika katika maendeleo ya nchi hii”aliongeza Profesa Wangwe.
Mbali na hayo Profesa Wangwe
ameshauri Serikali kuweka mfumo mzuri katika ukusanyaji kodi kwa
kurasimisha biashara ili mfumo huu wa EFD utumike kirahisi na pia
kutengenezwe mazingira mazuri ya biashara kwa kuweka mazingira rahisi ya
kuandikisha biashara kwani huchukua muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo
kasi ya kurahisisha utendaji na wafanyabiashara watalipa kodi kwa wingi
na uchumi utakua.
Pia Profesa Wangwe ametoa ushauri
kwa vyama vya upinzani kuacha na na maandamano yasiyo na tija na badala
yake wakae chini na kuzungumza na serikali ilikupata mwafaka na hivyo
amani iendelee kuchanua katika nchi hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni