Jenista Mhagama kufungua Maonesho ya wajasiriamali.
Katibu Mtendaji wa Baraza la 
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa wa kwanza kulia 
akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya 
wajasiriamali yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam , 
kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta  Binafsi nchini 
(TPSF) Bw. Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya 
Sekta  Binafsi nchini (TPSF)  Bw. Godfrey Simbeye kushoto akiongea na 
waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali 
yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu
 Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i 
Issa.
Picha Zote Na Ally Daud-Maelezo
………………………………………………………………
Na Ally Daud-Maelezo
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, 
Vijana, Ajira na Walemavu  Mhe. Jenista Mhagama anatarajiwa kufungua 
maonesho ya wajasiliamali yatofanyika Septemba 26 katika viwanja vya 
Mlimani City ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Ujasiriamali na ushindani
 Tanzania(TEEC) kwa kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji  Wananchi 
Kiuchumi (NEEC) pamoja na Taasisi ya Sekta  Binafsi nchini (TPSF) ili 
kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari
 leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa 
amesema kuwa maonesho hayo yatalenga kuwawezesha wananchi kuwa wabunifu 
katika sekta ya biashara ili kupiga hatua kufikia uchumi wa kati.
“Maonesho ambayo yatafanyika kesho
 ni kwa ajili ya wajasiriamali wote wakubwa, wa kati na wadogo ili 
kuwawezesha kiujuzi na kiushindani katika soko la biashara” alisema Bi. 
Issa.
Aidha Bi. Issa amesema kuwa siku 
hiyo kutakuwa na kliniki ya biashara kwa watu wote kutoka kwa wataalamu 
wa biashara ili kuweza kuwapatia mafunzo wajasiriamali wakubwa na wadogo
 ili waweze kupata mafanikio yao na jamii kwa ujumla kupitia biashara 
zao.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji 
wa Taasisi ya Sekta  Binafsi nchini (TPSF)  Bw. Godfrey Simbeye amesema 
kuwa maonesho hayo  yatawajengea wajasiriamali fursa za masoko kwa 
biashara nchini na Afrika kwa ujumla.
“kupitia maonesho hayo 
wajasiriamali watapata fursa ya kutengeneza masoko ya biashara zao kwa 
ubora zaidi nchini na afrika kwa ujumla ili waweze kujitangaza 
kimataifa” alisema Bw. Simbeye.
Aidha Bw. Simbeye amesema kuwa 
wana mpango wa kuwaelimisha wajasiriamali kwa wingi zaidi ili waweze 
kuwa wabunifu na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya biashara ndani 
na nje ya Tanzania.
Mbali na hayo Mkurugenzi Simbeye 
amesema kuwa anawakaribisha watu wote wajasiriamali wakubwa na wadogo 
kufika katika maonesho hayo ambayo hayana kiingilio ili waweze kupata 
ujuzi wa kutosha kwa maendeleo ya biashara zao na kuinua uchumi wa nchi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni