TaBSA KUWANOWA WACHEZAJI WACHANGA WA MPIRA WA MAGONGO
Dar es Salaam
CHAMA cha mchezo wa magongo nchini
(TaBSA) kwa kushirikiaa na wadau wa mchezo huo kutoka Marekani
kimeandaa kambi ya mafunzo ya majaribio kwa wachezaji vijana
yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya tarehe 2-4 Septemba mwaka huu.
Kambi hiyo ni sehemu ya maandalizi
ya Tanzania kwa ajili ya michezo ya olimpiki ya inayotarajiwa kufanyika
mwaka 2020 katika Jiji la Tokyo nchini Japan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa TaSBA, Bw. Alpherio Nchimbi
alisema mafunzo hayo yatawahusisha wanafunzi kutoka shule za Sekondari
za Azania, Kibasila, Temeke na Tiger Klub.
Nchimbi aliwataja wanafunzi 5
waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo hayo ni Djeskan Dihonga na Leodgar
Leonidas (Azania), Nathan Joram na Peter Pius (Kibasila) na Musa Mbugi
(Temeke) na Abdulwahid Anwar kutoka klabu ya Tiger.
Nchimbi aliwata taratibu za maandalizi za safari hiyo zimeanza ikiwemo kuomba ruhusa kutoka kwa Viongozi wa shule hizo.
“Endapo kijana atafanya vizuri
katika majaribio haya ni nafasi kwake kupata scholarship ya masomo na
mafunzo ya mchezo huu nchini Afrika kusini na marekani” alisema Nchimbi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni