WASHINDI WA DANCE BATTLE ZONE (MPAMBANO WA DANSI), KWA MKOA WA DAR ES SALAAM WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO
Mkurugenzi, UDO East Africa Ashraf
 Rwabigimbo akimkabidhi Amani Hamisi mfano wa hundi ya shilingi milioni 
moja mshindi wa shindano la dansi kutoka kundi la  BITZ – House of 
Kinetix  lililofanyika mwezi huu jijini Dar es salaam, katikati ni Idris
 SD Mkurugenzi wa Fedha UDO East Africa.
Mkurugenzi, UDO East Africa Ashraf
 Rwabigimbo akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya
 habari Maelezo jijini Dar es salaam kuhusu ushindi wa Amani Hamisi 
aliyekaa kushoto, kulia ni  Idris SD Mkurugenzi wa Fedha UDO East 
Africa.
…………………………………………………………………………
Dance Battle Zone ni shindano la 
Mpambano wa Dansi linalo andaliwa na kuendeshwa na United Dance 
Organization (UDO)- East Africa.
UDO East Africa ni sehemu ya 
Mtandao wa shirika linalo andaa mashindano ya dance duniani, linalo 
fahamika kama United Dance Organization (UDO) lenye makazi yake jijini 
Cardif Nchini Uingereza.
Shindano hili linawahusisha vijana
 wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea na linafanyika kwa awamu 
mbili na kwa upande wa Tanzania litafanyika katika awamu mbili, ya mkoa 
na awamu ya pili itakuwa ni ya Kitaifa na litashirikisha jumla ya mikoa 
mine (4) kwa kuanzia.
Kwa mkoa shindano hili limeanzia 
na mkoa wa Dar es Salaam, ambapo shindano hili lilizunduliwa rasmi na 
Mheshimiwa Mbunge wa Mikumi, Jospeh Haule almaarufu kama Prof J. mnamo 
August 7, 2016 na kumalizika 28 August, na Mshindi wa Dar es Salaam ni 
kundi la BITZ – House of Kinetix (Majina halisi ya wanakundi ni Beston 
Shaban na Amani Hamisi), amabao wamepata zawadi ya pesa taslimu shilingi
 za kitanzania  1,000,000/= (Milioni moja)
Mshindi wa pili ni Nadzz Lilbeast 
(Nadeem Nizar), mshindi wa tatu ni Tafa Makuzi, Mshindi wa nne ni Editoo
 Kinywele (Idris Hamza) na Mshindi wa tano ni Angels’ (Angel Nyigu na 
Abdully Ally). Washindi wote wata wakilisha Mkoa wa Dar es Salaam Katika
 shindano la Kitaifa April 2017. Pamoja na fedha taslimu pia washindi walipata medali za dhahabu na silva kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa tano
Baada ya Dar es Salaam, Dance 
Battle Zone litahamia katika mkoa wa Dodoma mwezi Septemba, ikifuatiwa 
na mkoa wa Arusha mwezi October na Zanzibar itakuwa ni mwezi December 
2016
Lengo la shindano ni kupata 
mshindi atakayewakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia ya UDO 
World Street dance Championships, yatakayo fanyika huko Glasgow 
Scotland, mwakani mwezi kama huu wa August 2017.
UDO East Africa ina sajili 
washiriki 20 kila mkoa litakapo fanyika shindano la dance battle zone. 
washiriki watashindana kwa round nne kwa mwezi, yaani mara moja kwa 
wiki. Mshindi wa kwanza wa kila Mkoa atazawadiwa pesa taslimu Sh Milioni
 1 ya kitanzania, pamoja na medali, mshindi wa pili hadi wa tano 
watapata medali na fursa ya kushiriki shindano la kitaifa. Ambapo 
mshindi wa kitaifa atapata fursa ya kushiriki shindano la dunia huko 
Glasgow Scotland, vigezo na masharti kuzingatiwa. Kila mshiriki wa dance
 battle zone atapewa cheti cha ushiriki.
Tunatoa wito kwa vijana wote wenye
 vipaji vya kucheza muziki wajitokeze na kushiriki shindano hili adhimu,
 fomu zinapatikana katika tovuti yetu ya www.udoeastafrica.com,
 pia katika ukumbi wa Maisha Basement, na Ofisi zetu zilizopo Kinondoni 
Road, mkabala na Bakwata. Dance ni kipaji, dance ni ajira, kuwa star 
kupitia dance battle zone.
Shindano hili linaletwa kwenu na 
UDO East Africa, kwa kushirikiana na Maisha Basement, Haak Neel 
Production, Mwakoba Associate, chini ya usimamizi wa Baraza la Sanaa la 
Taifa – BASATA.
UDO East Africa inawakaribisha wadau wote wanaopenda kushiriki na kudhamini shindano la Dance Battle Zone almaarufu kama Mpambano wa Dance. Wasiliana nasi kupitia barua pepe; info@udoeastafrica.com , simu namba; +255 653 88 44 81
UDO East Africa inawakaribisha wadau wote wanaopenda kushiriki na kudhamini shindano la Dance Battle Zone almaarufu kama Mpambano wa Dance. Wasiliana nasi kupitia barua pepe; info@udoeastafrica.com , simu namba; +255 653 88 44 81
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni