Mauzo soko la hisa yashuka kwa asilimia 34
Na Ally Daud-Maelezo
Idadi ya mauzo katika soko la hisa
Dar es salaam (DSE) imeshuka kwa asilimia 34 na kufikia shilingi
bilioni 2.2 kutoka shilingi bilioni 3.3 wiki iliyopita kutokana na
ukubwa wa idadi ya mauzo kushuka.
Katika taarifa iliyotolewa na
Afisa Mwandamizi wa Masoko DSE Bi. Mary Kinabo imesema kuwa idadi ya
mauzo hayo yameshuka kutokana na kupungua kwa idadi za hisa zilizouzwa
kutoka shilingi milioni 2.2 hadi kufikia shilingi milioni 1.3.
Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa
Benki ya CRDB imeendelea kuongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na
kununuliwa kwa asilimia 41 ikifuatiwa na Soko la hisa DSE ikiwa na
asilimia 36 na ya tatu ni Benki ya NMB yenye asilimia 9.
Taarifa hiyo iliendelea kueleza
kuwa ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 0.03 na kufikia
shilingi trilioni 22.7 kutoka trilioni 23.4 wiki iliyopita na ukubwa wa
mtaji wa makampuni ya ndani umeshuka kwa 0.01% na kufika Trilioni 8.3
kutoka trilioni 8.4 wiki iliyopita
Mbali na hayo taarifa hiyo
imeeleza kwamba licha ya mauzo kushuka lakini pia viashiria vya soko
katika sekta ya viwanda vimeshuka kwa alama imeshuka kwa alama 66.10
baada ya bei za hisa za TBL kushuka kwa 2.13% pamoja na kaunta za DSE
kwa asilimia na DCB kwa asilimia 14.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa
viashiria vya soko katika sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imebaki
kwenye hali yake ya wiki iliyopita baada ya bei za hisa za Swissport
kubaki shilingi 3,543.02.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni