Jumatano, 31 Agosti 2016

UONGOZI WA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO KATIKA ENEO LA MWENGE WAPINGA OPERESHENI UKUTA


2
Mwenyekiti wa  wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika halimashauri ya Kinondoni,Bw  Omary Hamis (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) akipinga wafanya biashara wake wasi kubali kurubuniwa na wanasiasa katika mambo ambayo hayana faida kwao (kulia) Sharifu Hasan.
1
Mwenyekiti wa  wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika halimashauri ya Kinondoni,Bw  Omary Hamis (katikati) akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, kushoto ni Katibu wa Ulinzi Shirikishi wa Wafanyabiashara wa eneo hilo, Dick Ponda, na kulia  Sharifu Hasan.
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
…………………………………………………………………………………………….
MWENYEKITI wa wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika halimashauri ya Kinondoni, Omary Hamis amewataka wafanya biashara wake wasi kubali kurubuniwa na wanasiasa katika mambo ambayo hayana faida kwao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam , alisema maranyingi vijana ndio wamekuwa wakishawishiwa kuandamana hivyo wao meona hakuna umuhimu wa kuandamana kwani kufanya hivyo hakuna faida kwao.
“Maranyingi vijana wamekuwa wa kishwawishika na wana siasa kuandamana kitu ambacho siyo chamsingi kwetu kama ambavyo tunashawishiwa tuandamane Septemba mosi mwaka huu eti kisa kuna Oparesheni Ukuta, hivi kwani huo ukuta unafaida gani kwetu, ifahamike kuwa hii nchi ni moja, Taifa letu n moja sisi ni wamoja hivyo tusikubali kufanya maandamano yasiyo na tija kwetu,” alisema Hamis.
Aliongeza kuwa Rais John Magufuli ameonesha nia ya dhati ya kupambana na maadui watatu amabao ni Maradhi, Ujinga na Umasikini hivyo hakuna sababu ya kuacha kumungamkono kutoka na juhudi anazo zifanya za kujenga Taifa hasa kwa kuwatetea wanyonge.
Naye Katibu wa Ulinzi Shirikishi wa Wafanyabiashara wa eneo hilo, Dick Ponda alisema Mfanyabiashara yoyote yule na vijana wote nchini atakama ni mwanachama wa Chadema au chama chochote kile asikubali kushwawishika kuandamana na Oparesheni ukuta kwani Rais wa nchi amekataza maandamano, na kufanya hivyo kutasabisha madhara makubwa kwao.
Alisema umefika wakati sasa vijana kujituma kwa bidii katika kufanya kazi, muda uliopo ni wakufanya kazi na wala si siasa kama baadhi ya vyama wanavyo fanya, Rais John Magufuli haangali chama katika utendaji wake hivyo kila mtu anapaswa kuweka maswala ya chama chake pembeni.
Kwa upande wake mmoja kati ya Wafanyabiashara hao, Fadhili Leuteni alimpongeza mwenyekiti wao kutokana na ujasili wake wakuwakemea wafanyabiashara wa eneo hilo.
“Mwenyekiti wetu pamoja na viongozi wake wapo sahihi kwasabu maranyingi sisi ndio tumekuwa tukitumiwa katika mambo ya uchochezi, hivyo na waomba wezangu wasikubali kulubuniwa na wanasiasa kwani tutapata madhara makubwa ni vyema kujiepusha,” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni