Watanzania tupaze sauti kukataa maandamano ya Septemba Mosi – Cheyo
Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party
 (UDP) John Momose Cheyo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo 
pichani) kuhusu hali ya kisiasa nchini katika mkutano uliofanyika katika
 ukumbi wa Idara ya Habari – Maelezo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto 
ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – Maelezo Tiganya Vicent.
Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party
 (UDP) John Momose Cheyo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo 
pichani) kuhusu hali ya kisiasa nchini katika mkutano uliofanyika katika
 ukumbi wa Idara ya Habari – Maelezo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka 
kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – Maelezo Tiganya 
Vicent na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho Goodlucky Ole Medeye.
………………………………………………………………………………
Na: Lilian Lundo -MAELEZO
Dar Es Salaam
Mwenyekiti  wa Chama cha UDP John 
Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na kukataa maandamano ya 
Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na Chama cha Demokrasia 
(CHADEMA).
Cheyo ameyasema hayo leo jijini 
Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo 
wake juu ya  maandamano hayo.
“Watanzania wenzangu jambo la 
kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si jambo zuri, wote 
tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya Septemba Mosi,” 
alisisitiza Cheyo.
Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali
 ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua migogoro, kama vile meza ya 
mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo yanachochea vurugu na hata 
kutishia amani ya nchi.
Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi 
linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii uwepo, kwani Polisi wapo 
kwa mujibu wa Sheria na  Katiba. Ikiwa Chama hicho hakikuridhika na 
katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la 
Polisi.
Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais
 Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za  kutatua matatizo 
mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo viongozi wengi wa 
Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa  kutokana na kujihusisha na 
masuala ya rushwa.
Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka 
watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili aweze kutimiza ndoto 
zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.
Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa 
Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) 
 na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi lolote. Amewataka viongozi 
hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la amani kwa Watanzania na 
Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni