MRI, CT-Scan Zapiga Mzigo Saa 24 Muhimbili, Wagonjwa 41,101 Wapimwa
Mgonjwa
 akiwa katika mashine ya MRI LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili 
(MNH). Pembeni ya mgonjwa ni Mtaalamu wa Mionzi, Medard Mallya 
akimsaidia mgonjwa kukaa vizuri kwenye mashine hiyo.
…………………………………………………………………………………………..
Na John Stephen, MNH
 Hospitali ya Taifa Muhimbili 
(MNH) inaendelea kutoa huduma bora hasa ya vipimo kwa wagonjwa 
mbalimbali na kufanikiwa kupima wagonjwa 41,101 katika mwaka 2015/2016 
kutoka wagonjwa 32,010 waliopimwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa 
Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Buberwa 
Aligaesha imeeleza kwamba mashine zinafanya kazi vizuri na kwamba hakuna
 mashine mbovu hadi kusababisha wagonjwa kukosa huduma za vipimo.
“Hospitali inahakikisha kila 
mgonjwa anayehitaji vipimo anapata na kwa gharama nafuu. Kama mashine 
ilisimama kufanya kazi tangu Januari hadu Juni, 2016 ni kwa muda wa kati
 ya siku moja hadi mbili kupisha matengenezo kinga,” amesema Bwana 
Aligaesha katika taarifa yake aliyoitoa LEO kwa vyombo vya habari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni