Bodi Mpya Yaanza Kazi Rasmi Muhimbili
Msimamizi wa Chumba cha wagonjwa
wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Trustworthy Majuta akieleza
mafanikio na changamoto kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Charles Majinge (wa tatu kulia) na
wajumbe wa bodi hiyo. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa Mapafu kwa wagonjwa
waliozidiwa, Dk Alex Masau, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,
Isaya Charles na Msimamizi wa Jengo la Mwaisela, Adelini Jacob.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Charles
Majinge, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Charles (mwenye
koti) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence
Museru wakiwa katika chumba cha CT-Scan ambako wagonjwa wanachukuliwa
vipimo.
Mkuu wa Kitengo cha Ufuaji, Linah
Kinabo akiwaeleza wajumbe wapya wa bodi ya Muhimbili jinsi wanavyofanya
kazi na changamoto mbalimbali katika kitengo hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Muhimbili, Profesa Lawrence Museru (kulia), Mwenyekiti mpya wa Bodi,
Profesa Charles Majinge na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk
Grace Magembe wakiendelea na ziara katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Pua,
Koo na Sikio, Dk Edwin Liyombo akiwaeleza jambo wajumbe wa bodi hiyo
walipoetembelea hospitali hiyo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa
Hospitali hiyo, Makwaia Makani (kushoto) na Mstahiki Meya wa Jiji la
Dar es Salaam, Isaya Charles wakiingia kwenye wodi za wagonjwa wenye
matatizo ya afya ya akili.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharula na Ajali katika Hospitali ya Muhimbili, Dk Juma Mfinanga
akiwaeleza wajumbe wa bodi kazi zinazofanywa na idara hiyo.
Sehemu ya Jengo la Idara ya
Magonjwa ya Dharula na Ajali likiwa limekarabatiwa kwa ajili ya kutoa
huduma bora na kisasa kwa wagonjwa mbalimbali. (Picha na John Steven
MNH)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni