Serikali, wadau wakutana kujadili mapendekezo ya kulinda na kukuza Haki za Binadamu Nchini
Mkurugenzi Masuala ya Katiba na 
Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah 
Mwaipopo akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati
 wa ufunguzi wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali 
wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya 
haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza 
la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi
 mbalimbali za Kiraia wakimsikiliza Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki
 za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah 
Mwaipopo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kujadili mapendekezo 
yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya 
utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa
 kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa matafa, Leo 
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Masuala ya 
Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. 
Nkasori Sarakikya akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi 
mbalimbali za Kiraia mara baada ya ufunguzi wa kikao cha kujadili 
mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa 
ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa 
mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa 
matafa, Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba
 na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi hiyo Bi. Sarah Mwaipopo.
…………………………………………………………………
Serikali,kupitia Ofisi ya 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo imefanya  kikao maalumu cha wadau 
kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na asasi za kiraia kwa lengo la 
kuwafahamisha kuhusu kujadiliwa kwa Taarifa ya pili ya nchi ya 
utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa
 kipindi maalum (The Universal Period Review).
Vilevile kikao hicho kitatoa fursa
 ya kujadili kwa kina na kuyapatia misismamo ya awali kama wadau, 
mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa 
Mataifa kwa Serikali mnamo mwezi Mei 2016 , na kuainisha sababu ambazo 
zinafaa kwa mapendekezo yaliyoahirishwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu 
kabla ya kupitishwa rasmi kuwa  taarifa ya nchi itakayowasilishwa kwenye
 Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kabla ya terehe 9 
Septemba 2016.
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi 
wa masuala ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwansheria Mkuu
 wa Serikali, Bi Sarah Mwaipopo ameeleza kuwa kikao hicho ni hatua 
muhimu kkatika mfumo wa maandalizi ya taarifa za usimamizi na 
utekelezaji wa haki za binadamu nchini ambao umekua ukishirikisha wadau 
wote kutoka Wizara,Idara na Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi zisizo
 za kiserikali ambapo amesisitiza wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano
  na kutimiza wajibu wao  ipasavyo.
“Sote tutambue na kuzingatia 
kwamba masuala ya haki za biandamu ni mtambuka na kila mtu ana wajibu wa
 kutekeleza na kuyasemea katika eneo lake”alisema Bi Sarah
Halikadhalika,kwa niaba ya 
Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekua ikiratibu 
kikamilifu maandalizi  na uwasilishwaji wa  Taarifa  zote za masuala 
yote ya  haki za binadamu kwa kuzingatia mikataba ya Haki za Binadamu 
ambayo Tanzania imeridhia na utekelezaji wa jukumu hili umeanishwa 
katika Ibara ya 59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na 
Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa 
Serikali Sura ya 268, kifungu cha 14(f) ambayo ni;
 kuratibu masuala ya uaandaaji na 
utoaji wa taarifa za nchi za utekelezaji wa Mikataba ya Kikanda na 
Kimataifa ya haki za binadamu amabyo nchi imeridhia ikiwemo masuala yote
 ambayo yanahitaji utolewaji wa taarifa za aina hiyo na kuziwasilisha 
kwenye vyombo husika vya Kikanda na Kimataifa kwa ajili ya majadiliano.
Kikao hicho ambacho kitafanyika 
kuanzia tarehe 30 -31 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa 
na wadau kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao ni  Ofisi ya Mwanasheria
 Mkuu wa Serikali,Jukwaa la Katiba Tanzania,Chama cha Watu wenye Ualbino
 Tanzania,MISA-TAN,PINGOS’ FORUM,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya 
Siasa,Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama ya Tanzania,Uhamiaji,Tume ya 
Haki za Binadamu na utawala bora, Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA),
 Shrikisho la Watu wenye ulemavu Tanzania( SHIVYAWATA) na Msajili wa 
Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Kwa upande wa Zanzibar ni Wizara ya 
Kilmo na Mifugo, Wizara za Afya,Mifugo, Kazi,Vijana Wazee,Ofisi ya 
Mwansheria Mkuu, Jumuia ya Wanawake Wanasheria,Tume ya Uchaguzi
Utaratibu wa Mapitio kwa kipindi 
maalum (The Universal Periodic Review) wa masuala ya haki za binadamu 
ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2006 kwa lengo la kuzifanyia
 mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania 
ikiwa miongoni, kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa masuala ya kulinda
 na kukuza haki za binadamu nchini mwao
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni