WANAFUNZI WA CHUO CHA DIPLOMASIA WAMNUNULIA MWENZAO VIFAA VYA KUMSAIDIA KUSIKIA, ANA UWEZO MKUBWA DARASANI PAMOJA NA MATATIZO YAKE
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Diplomasia
Dk Bernald Achiula akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo wakati
akishukuru wanafunzi wa chuo hicho kwa michango yao waliyochanga ili
kumsaidia mwanafuzni mwenzao Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ana matatizo
ya kusikia, wanafunzi hao wamechanga Fedha na kumnunulia mwenzao Vifaa
vya kumsaidia kusikia vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki
tano, Kulia ni Mwanafuzni Shinuna Salum Nyamkokwa ambaye ameelezewa
kuwa ana uwezo mkubwa katika masomo yake darasani pamoja na kutokuwa na
uwezo wa kusikia, na Katikati ni Neema Zawadi Henjewele Makamu wa Rais
Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia.
Neema Zawadi Henjewele Makamu wa
Rais Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia akielezea kwa
waandishi wa habari kuwa kitu kilichowafanya wanafunzi wa chuo hicho
kumchangia mwanafunzi mwenzao Shinuna Salum Kulia ni kutokana na uwezo
wake katika masomo pamoja kuwa tatizo la usikivu linalomkabili
Mwanafuzni huyo Shinuna Salum
Nyamkokwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea
kuhusu msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema awali kichwa kilikuwa
kinamuuma sana lakini kwa sasa hakiumi tena.
Gordian Kilave Mkuu wa Idara ya
Lugha Chuo cha Diplomasia akielezea matatizo yaliyokuwa yakimkuba na
kumsumbua mwanafunzi Shinuna Salum kabla ya kupatiwa vifaa hivyo ambavyo
ninamsaidia kusikia kwa sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni