Baraza la ushauri latoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda kwenye insha
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta Mawasiliano mhandisi Dkt. Maria Sasabo kushoto akizungumza wakati wa hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano, kulia ni Katibu wa Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bi. Mary Shao Msuya.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Bw. Stanley Mwabulambo akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo kuzungumza na wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi za jijini Dar es Salaam walioshinda shindano la uandishi wa insha kuhusu haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu Bw. Omari Abbas kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Ualimu (DUCE) akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za sekondari Bw, Ramadhani Mohamed kutoka Shule ya sekondari ya Kibasila akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
Mshindi wa kwanza wa insha kwa upande wa Shule za Msingi Jane Michael Andrew kutoka shule ya msingi ya Mbuyuni akipokea zawadi ya cheti ya mshindi wa kwanza wa insha kutoka kwa Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) mhandisi Dkt. Maria Sasabo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni