NETBALL TANZANIA YAANZA VYEMA MASHGINDANO YA MAJESHI
Mchezaji Nasra  Suleiman wa 
Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao 
wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za  Afrika Mashariki katika 
Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 (Picha na 
Selemani Semunyu)
Mchezaji  Faraja Malaki wa 
Tanzania akiwania mpira mbele ya Wachezaji wa Uganda katika michezo wao 
wa Kwanza wa mashindano ya Majeshi kwa nchi za  Afrika Mashariki katika 
Uwanja wa Amahoro Nchini Rwanda Tanzania ilishinda 29-27 (Picha na 
Selemani Semunyu)
Mchezaji  Veronica Patrick wa 

……………………………………………………………………………………………….
Na Selemani Semunyu JWTZ
Timu ya Mpira wa Pete Netball ya
 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ime3rejesha heshima yake baada 
ya Kuwafunga mabingwa Watezi  wa Michuano hiyo kwa Mpira wa Pete Uganda 
kwa magoli 29 kwa 27.
Katika Mchezo huo uliokuwa wa 
Vuta nikuvute  na rabsha za hapa na pale zilizizojitokeza kabla wakati 
na Baada ya Mchezo huo ambao ulikuwa na Upinzani Mkali kutokana na 
historia ya Timu hizo.
Katika Robo ya Kwanza Tanzania 
ilimaliza ikiongoza kwa magoli saba kwa Sita huku Timu zote zikicheza 
Mchezo wa kuviziana lakini uliojaa nguvu na kukamiana miongoni mwa 
Wachezaji.
Katika Robo ya Pili Tanzania pia
 ilimalizai ikiwa mbele kwa mabao 13 kwa 11 kukiwa na tofauti ya magoli 
mawili tofauti na robo ya kwanza ambayo ilimalizika kwa tofauti ya goli 
moja.
Robo ya Tatu Uganda walikuja na 
kusawazisha na kasha kuongeza na hivyo kumaliza kwa ushindi wa magoli 20
 kwa 19 ya Tanzania  na kuwafanya Tanzania kwenda kujiuliza.
Hatimaye robo ya Mwisho 
ikamalizika na Timu ya Tanzania kuibuka na Ushindi na hivyo kuwatisha 
Mabingwa wa mwaka uliopita pengine utarejea kwa Tanzania
 Kwa Upande wa Nahodha wa Timu 
hiyo Dorita Mbunda alisema mechi yao na Uganda wamecheza kama fainali 
kutoka na historian a kuahidi kujipanga kwa ajili ya kuwakabili Kenya. 
Kwa upande wake Nahodha Uganda 
Lilian Ajio amelalalimika Waamuzi kutoelewa Sheria Mpya za Mchezo huo 
hali iliyopelekea wakati mwingine kutokuwa na maamuzi sahihi.
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni