Mabalozi watembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya 
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi akizungumza na 
mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania. Kulia ni 
Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Edzai Chimonyo. Mabalozi hao 
wameitembelea taasisi hiyo ili kuona shughuli mbalimbali za kitibabu na 
wamehahidi kuwenda kupatiwa matibabu kwenye taasisi hiyo badala kwenda 
nchi nyingine ikiwamo Afrika Kusini kupatiwa huduma za magonjwa ya moyo.
 
Mabalozi wa nchi za Afrika 
nchini Tanzania wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya 
Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohammed Janabi baada ya kuitembelea 
taasisi hiyo LEO.
Profesa Janabi akizungumza na mabalozi katika taasisi hiyo LEO. 
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na mabalozi kwenye taasisi hiyo LEO.
Mabalozi hao wakiwa katika chumba cha upasuaji.
Mabalozi hao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni