MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MJINI MBABANE SWAZILAND TAYARI KWA MKUTANO WA 36 WA SADC
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwasili kwenye ardhi ya mji wa Mbabane nchini Swaziland tayari
kuhudhuria mkutano wa 36 wa SADC wa Wakuu wa nchi na Serikali ambao
utafanyika tarehe 29 Agosti mjini hapo.
Sehemu ya Mabinti wa Swaziland wakiimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokelewa na ngoma mbali mbali mjini Mbabane nchini Swaziland.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kushoto) akizungumza na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Phiwayinkhosi Mabuza wa Swaziland ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha
mara baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mfalme
Mswati III.
………………………………………………………
………………………………………………………
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewasili mjini Mbabane – Swaziland leo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano
wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika- SADC.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo ambao utafanyika
tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya
Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Mkutano
huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa wakuu wa nchi na serikali wanaounda
Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili kwa kina hali ya
siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro kwa ajili ya
kujiunga na SADC.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri
wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa
Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Amina Salum Ali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni