MKUTANO WA VYAMA VYA SIASA WAPIGWA KALENDA -VUAI ALI VUAI
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Vyama vya Siasa,Vuai Ali Vuai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichan) juu ya kusogeza mkutano wa vyama vya siasa leo jijini Dar es
Salaam, kushoto ni Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya fedha ya baraza la
vyama vya siasa, Constatine Akitanda.
Msajili wa Vyama vya Siasa,
Jaji Mstaafu, Francis Mutungia akisisitiza juu ya umuhimu wa mkutano wa
vyama vya siasa utaofanyika Septemba 3 hadi 4 kwaka huu jijini Dar es
Salaam mkutano uliofanyika katika Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa leo
jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………….
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BARAZA la vyama vya Siasa
limesogeza mbele mkutano wa kujadili sintofaham iliyojitoeza kwa baadhi
ya vyama vya siasa na kusababisha kuwepo kwa hofu, na taharuki kwa
wananchi.
Mkutano huo ulitangazwa kufanyika Agasti 29 hadi 30 na kusogezwa kufanyika Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi habari
jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,
Vuai Ali Vuai amesema kusogeza mbele kwa mkutano huo umetokana na kutaka
kutoa muda kwa wadau ili waweze kujiandaa.
Amesema kuwa mkutano huo ni muhimu
sana kwa wadau kukutana na kujadili mambo yaliyojitokeza na kuweka sawa
kwa mstakabali wa taifa.
jukwaa la viongozi wa kitaifa wa
vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadiliana masuala yanayohusu
demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa nchini kwetu
Amsema kila chama cha siasa
kinawakilishwa na viongozi wawili wa ngazi kitaifa katika Baraza la
Vyama vya Siasa, ambapo kiongozi mmoja anapaswa kutoka Tanzania Bara na
mwingine Zanzibar.
Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
wa Baraza huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Baraza la Vyama
vya linaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za zilizotungwa na Baraza.
Baraza la vyama vya siasa lina majukumu ya kuishauri msajili
wa vyama vya siasa kuhusu migogoro baina ya vyama vya siasa,kumshauri
Msajili wa vyama vya siasa kuhusu masuala yenye masilahi ya kitaifa
yanayohusu vyama vya siasa na hali ya siasa nchini.
Aidha amesema kazi ya baraza hilo kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa,kushauri kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.
Aidha amesema kazi ya baraza hilo kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa,kushauri kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.
Baraza hilo linaweza kumtaarifu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala yoyote yanayohusu utendaji wa chama chochote cha siasaKamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti wa Baraza, Makamu Mwenyekiti wa Baraza, wenyeviti wa kamati nne za Baraza na katibu wa Baraza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni