Utumishi yapokea vijana wa kujitolea kutoka Japani
Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais
  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Bi. Susan Mlawi 
 alisema hayo mapema leo katika ukumbi wa mikutano wa Utumishi wakati wa
 hafla fupi ya kuwakaribisha watalaam wa kujitolea kutoka Japani.
“Tangu mwaka 1967 hadi sasa zaidi
 ya vijana wa Japani 1,500  wameshafika  nchini na kufanya  kazi za 
kujitolea katika maeneo mbalimbali hata katika mazingira magumu” Bi. 
Mlawi alisema na kuongeza kuwa  kunufaika huko kwa Tanzania kunatokana 
na ushirikano baina ya Serikali ya Japani na Serikali ya Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania.
Alisema Tanzania itaendelea 
kudumisha ushirikiano huo  na Japani  ili kuendelea kunufaika  hasa 
katika suala zima la kujengewa uwezo katika sekta ya elimu na maendeleo 
ya jamii , sekta ambazo pia  zimepewa kipaumbele  katika Awamu ya Pili 
ya  Mpango wa Serikali wa  miaka Mitano (5) wa Maendeleo inayoanza mwaka
 2016/17 na kumalizika mwaka 2021 /22.
Kwa upande wake,  mwakilishi mkuu
 wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japani (JICA) nchini  Tanzania 
 Bw. Toshio Nagase  alisema wataalam hao ambao wako sita (6) 
 watafanyakazi ya kujitolea katika sekta ya elimu kwa miaka miwili na 
kwa kipindi hicho wanaamini Watanzania watakuwa wamenufaika na ujuzi 
toka kwa vijana hao.
Alisema watajitolea kufundisha 
masomo ya Sayansi, Hisabati, Masuala ya Maendeleo ya Jamii  na Michezo 
 katika shule za Sekondari , Shule za Msingi  na Ofisi za  Maendeleo ya 
Jamii katika Mikoa ya Morogoro, Pwani , Mtwara , Dodoma na Dar es 
salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni