MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, MHE. GEORGE MASAJU AVIASA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU KATIBA YA NCHI
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh.
George Masaju akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
wakati alipoelezea masuala mbalimbali ya kisheria yanayozuia
maandamano ya Ukuta yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Mendeleo
CHADEMA, kulia ni Asiatu Msuya Ofisa habari wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali.
………………………………………………………………………………..
Na Hassan Silayo
MAELEZO -Dar es Salaam.
VYAMA vya siasa nchini
vimetakiwa kutumia vyema haki zao za msingi zilizoanishwa katika katiba
badala ya kutumia nguvu ubabe na kupelekea kutishia hali ya amani ana
utulivu iliyopo nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju wakati wa
mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari akizungumzia kuhusu wajibu
wa utii wa sheria na kudumisha amani nchini.
Mhe. Masaju alisema kumekuwa na
baadhi ya wanasiasa wanaotoa vitisho vya kuitisha mikutano kinyume na
taratibu za kisheria kwa kisingizio cha haki za kikatiba jambo ambalo
sio kweli.
“Napenda kuvishauri vyama vya
siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio
cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola
kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”.
Masaju aliwataka Wanasiasa kuwa
wakweli na kuacha kuwapotosha wananchi kuwa wananyimwa haki ya kufanya
mikutano kwani wapo baadhi yao wanaofanya mikutano katika majimbo yao
baada ya Jeshi la Polisi kujidhirisha kwamba kutakuwa na hali ya amani
na utulivu”. Alisema Mhe. Masaju.
Aidha Masaju alipongeza juhudi
zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa dini nchini kwa jitihada
wanazofanya za kushauri katika kufika muafaka wa hali ya kisiasa nchini
na kuwashauri kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao.
Akitoa ufafanuzi wa tamko la
baadhi ya vyama vya upinzani kutaka serikali kuvifuta vyama hivyo Mhe.
Masaju alisema kuwa suala hilo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa sababu katiba hiyo inaruhusu mfumo wa vyama
vingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni