SERIKALI YA MKOA WA IRINGA YAPONGEZA TUZO YA UBORA WA MAZIWA KUTOKA KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Richard Kasesela (wa tatu kushoto )ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa
akiongoza washiriki wa warsha ya wiki moja ya kilimo biashara
yaliyoandaliwa na Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na
kilimo (UNCTAD) kwa ufadhili wakampuni ya Asas Dairies Ltd na SAGCOT
kupongeza ubora wa maziwa ya kampuni ya Asas Dairies Ltd baada ya
kushinda tuzo ya ubora wa bidhaa za maziwa Afrika tuzo ya ARSO leo
wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ,wengine pichani kutoka kushoto
wa kwanza ni Meneja maendeleo na biashara Roy Omulo ,mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Ahmed Abri na mwakilishi wa
katibu mtendaji wa SAGCOT CTF Mbosela John Mosela kulia
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Richard Kasesela ( mwenye suti katikati) akiwasili eneo la warsha
kwa ajili ya ufungaji kushoto kwake ni mkurugenzi wa Asas Dairies Ltd
Ahmed Abri na washiriki wengine
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Richard Kasesela (wa tatu kushoto )ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa
akiongoza washiriki wa warsha ya wiki moja ya kilimo biashara
yaliyoandaliwa na Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na
kilimo (UNCTAD) kwa ufadhili wakampuni ya Asas Dairies Ltd na SAGCOT
kufungua maziwa kabla ya kupongeza ubora wa maziwa ya kampuni ya Asas
Dairies Ltd baada ya kushinda tuzo ya ubora wa bidhaa za maziwa
Afrika tuzo ya ARSO wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ,wengine
pichani kutoka kushoto wa kwanza ni Meneja maendeleo na biashara
Roy Omulo ,mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Ahmed
Abri na mwakilishi wa katibu mtendaji wa SAGCOT CTF Mbosela John
Mosela kulia
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Richard Kasesela (katikati)ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa akifunga
warsha ya wiki moja ya kilimo biashara yaliyoandaliwa na Shirika la
umoja wa mataifa linalojishughulisha na kilimo (UNCTAD) kwa ufadhili
wakampuni ya Asas Dairies Ltd na SAGCOT kwa wafugaji 35 kutoka mkoa
wa Iringa , Mbeya na Njombe leo ,kushoto wa kwanza ni meneja biashara na
maendeleo wa kampuni ya maziwa ya Asas akifuatiwa na mkurugenzi wa
kampuni ya Asas Dairies Ltd Ahmed Abri na kulia ni mwakilishi wa
katibu mtendaji wa SAGCOT CTF Mbosela John Mosela
………………………………………………………………….
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI ya mkoa
wa Iringa imeipongeza kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya
mkoani Iringa kwa kushinda tuzo ya (ARSO) kwenye mashindano ya
kimaifa ya nchi za Africa ya ubora wa bidhaa za maziwa kuwa ni tuzo
yenye heshima kubwa kwa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla .
Pamoja na pongezi hizo pia
imepongeza jitihada zinazofanywa na kampuni ya Asas Dairies Ltd
kwa kuwawezesha mafunzo mbali mbali wafugaji wa mikoa ya Mbeya ,
Njombe na Iringa kubadili ufugaji wa kienyeji na kufuga
kibiashara zaidi .
Huku ikiwataka wenye viwanda
vya usindikaji maziwa kujenga utamaduni wa kuwafikia wafugaji na
kuwapa elimu ili kuwezesha bidhaa zao za maziwa kuendelea kuwa
zenye ubora zaidi na ikiwezekana kuwawezesha kupata vifaa vya
kisasa vya kukamulia maziwa.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa
Richard Kasesela aliyasema hayo leo kwenye ukumbi wa Asas mjini hapa
wakati wa ufungaji wa mafunzo ya wiki moja kwa wafugaji 35 kutoka
Iringa , Mbeya na Njombe mafunzo yaliyoandaliwa kilimo biashara
yaliyoandaliwa na Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na
kilimo (UNCTAD) kwa ufadhili wakampuni ya Asas Dairies Ltd na
SAGCOT CTF
Alisema kuwa kampuni hiyo
imeupa mkoa wa Iringa heshima kubwa na kuwa ukiacha mashindano mbali
mbali ya maziwa kwa viwanda vya ndani ya Tanzania kampuni hiyo
imekwisha shinda mara nne sasa jambo ambalo ni la kujipongeza na
kujivunia kuwa bidhaa zinazozalishwa ni bora na hivyo si wakati wa
watanzania kukimbilia bidhaa za nje na kuacha zinazozalishwa ndani ya
nchi .
Kasesela ambae pia ni mkuu wa
wilaya ya Iringa alisema kuwa mbali ya wadau na wawekezaji waliopo
katika wilaya yake na mkoa wa Iringa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni