MBWANA SAMATTA AIPELEKA GENK HATUA YA MAKUNDI LIGI YA EUROPA
Mchezaji
wa kitamataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya
kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Hii ni baada ya klabu yake ya KRC
Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla wa 4-2 mechi ya kufuzu hatua ya
makundi dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.
Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa Alhamisi jioni.
Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.
Samatta alifungia klabu yake bao
la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda
mfupi baada ya mapumziko.
Samatta pia alioneshwa kadi ya manjano dakika ya 69.
Droo ya hatua ya makundi itafanywa mjini Monaco baadaye leo Ijumaa mwendo wa saa tisa saa za Afrika Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni