Tanzania kuwa mwenyekiti TROIKA
Mheshimiwa Rais  Dk. John Pombe Magufuli
…………………………………………………………………………………………………..
Na. Immaculate Makilika na Abushehe Nondo- MAELEZO
Dar es Salaam
Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine 
Mahiga amesema Tanzania imepokea nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya TROIKA
 ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa 
Afrika (SADC) inayosimamia masuala ya Ulinzi na Usalama.
Akizungumza
 na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Balozi Mahiga alisema 
Tanzania imepata nafasi hiyo wakati wa Mkutano wa SADC uliojadili masula
 ya Ulinzi na Usalama uliofanyika  hivi karibuni mjini Maputo, Msumbiji.
“Mheshimiwa
 Rais John Pombe Magufuli atapokea nafasi hiyo ya kuwa mwenyekiti wa 
TROIKA kutoka kwa Rais wa sasa wa Msumbiji, Filipe Nyusi, nafasi 
inayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja” alisema Balozi Mahiga.
Aliongeza kuwa Mkutano huo wa TROIKA unatarajiwa kufanyika Agosti 29 na 30 mwaka huu huko Mbabane nchini Swaziland.
Aidha,
 Balozi Mahiga alisema kuwa SADC ni jumuiya iliyopiga hatua katika 
kusimamia masuala ya ulinzi, usalama na diplomasia jambo ambalo haliko 
katika jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kusaidia kutatua masuala 
yanayohusu hali tete za usalama katika ukanda huo.
Kwa
 mujibu wa Waziri Mahiga alisema mkutano wa TROIKA ni sehemu ya 
maandalizi ya kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini 
mwa Afrika kinachotarajiwa kufanyika baadae mwezi huu ambapo, taarifa ya
 hali tete ya usalama ya nchini Lesotho itatolewa.
Waziri
 Mahiga, alisema katika mkutano wa SADC uliofanyika mapema mwezi huu 
Maputo Msumbiji uliitaka nchi ya Lesotho kutekeleza masuala kadhaa 
katika kutafuta suluhu ya matatizo nchini humo, ikiwemo kufanya mageuzi 
ya katiba, mageuzi ya sekta ya ulinzi na usalama pamoja na kufanya 
marekebisho katika sekta ya utawala.
Mkutano huo wa SADC, vilevile unatarajiwa kujadili changamoto mbalimbali  zinazoikabili  jumuiya hiyo ikiwemo  mgogoro
 wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia kuibuka 
kwa makundi mbalimbali yanayohatarisha amani mashariki mwa nchi hiyo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni