NBS yapokea msaada wa Bil. 25 kwa ajili ya watoto
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Ashatu Kijaji akionyesha Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa
Tanzania mbele ya wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa
uzinduzi wa taarifa hiyo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Ashatu Kijaji akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa takwimu hawapo
pichani wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa
Tanzania jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa takwimu
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji hayupo
pichani wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa
Tanzania jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………
Na Ally Daud-Maelezo
Tume ya Taifa ya Twakimu (NBS)
imepokea msaada wa shilingi bilioni 25 kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili
ya kusaidia kuboresha tasnia ya takwimu kuhusu haki za watoto nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya
uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji amesema kuwa amepokea
msaada huo kwa nia ya kuendeleza tasnia ya takwimu nchini na kusaidia
malengo ya nchi ya miaka mitano.
“Tumepokea msaada huu kwa furaha
na hamasa kubwa katika kufikia lengo letu la kuboresha na kukuza tasnia
ya takwimu nchini ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya
maendeleo ya miaka mitano ya nchi yetu”. Alisema Mhe. Kijaji.
Aidha Mhe. Kijaji amesema kuwa
Wizara yake imewapa kipaumbele watoto kwa kutenga shilingi. Bilioni 18
kila mwezi ili kuwasaidia katika mambo muhimu ya kila siku hususani
elimu bora, makazi na malazi.
Mbali na hayo Mhe. Kijaji
ameshukuru na kuwapongeza Umoja wa ulaya kwa msaada huo na kuwataka
wasichoke kuwa nao pamoja katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu
ya mwaka 2030.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Balozi
wa Umoja wa Ulaya Bw. Eric Beaume Amesema kuwa msaada huo sio mwisho
wao kwani wanapenda kazi ya NBS na matokeo yake hivyo wapo tayari kutoa
kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha tume hiyo kutoa takwimu zenye uhakika
kwa maendeleo ya Tanzania.
Bw.Beaume amesema kuwa Umoja wao
utakua bega kwa bega na Tanzania katika kutoa misaada ili kusaidia haki
zote za watoto ili kujenga taifa lenye tija na muamko wa kimaendeleo
kutokana na takwimu zitokanazo na tume hiyo.
Aidha Bw. Beaume ameongeza kuwa
Umoja wao upo tayari kusaidia Nyanja za kilimo, Nishati katika maeneo ya
vijijini ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kufikia
malengo ya maendeleo endelevu kwa miaka mitano ijayo.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa
NBS Dkt. Albina Chuwa amesema kutokana na msaada huo wamepata hamasa
kubwa kwa tume hiyo kuweza kupambana na kupata takwimu yakinifu
zitazopelekea kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yahusuyo jamii
nchini na kufikia malengo ya miaka mitano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni