POLISI KUBORESHA VITUO VYAKE VYA AFYA.
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na
Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua
kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi
na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la
JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika
mkoani Dodoma.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Naibu Inspekta Jenerali wa
Polisi, Abdulrahman Kaniki akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa
kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu unaotekelezwa na
Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na tano hapa nchini
kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la JSI-AIDS Free tawi la
Tanzania.Mkutano huo wa siku tatu unafanyika mkoani Dodoma.Kulia ni
Mganga mkuu wa Polisi Dk.Janda Lushina na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Lazaro Mambosasa
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) Baadhi
ya Maofisa wa Polisi ambao ni Washiriki wa Mkutano wa kutathmini mradi
wa kupambana na ukimwi na kifua kikuu ndani ya Jeshi la Polisi
wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani Dodoma.Mradi
huo unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi na
tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la
JSI-AIDS Free tawi la Tanzania. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Dodoma
Jeshi la Polisi nchini
litaendelea kuboresha vituo vyake vya afya ili kuwawezesha Askari kupata
huduma zilizo bora jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi wakiwa na
afya pamoja na morali katika kupambana na uhalifu nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki Mkoani Dodoma wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini mradi wa kupambana na ukimwi na kifua
kikuu unaotekelezwa na Jeshi la Polisi katika vituo vyake vya Afya kumi
na tano hapa nchini kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la
JSI-AIDS Free tawi la Tanzania.
Kaniki alizitaja juhudi
zinazoendelea kuchukuliwa kuwa ni pamoja na kuboresha majengo, kutoa
mafunzo kwa watendaji pamoja na kuhakikisha kuwa hospitali za Polisi
zinakuwa na vifaa bora kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Wizara ya
Afya .
Aidha alitoa wito kwa Shirika
la JSI-AIDS Free kuongeza wigo wa huduma zake katika vituo vngine
ambavyo havijafikiwa na mradi huo hapa nchini ili kuhakikisha kuwa kila
mahali palipo na kituo cha Afya cha Polisi kunakuwepo na mradi huo ambao
umesaidia sana askari na watumiaji wengine wa huduma hizo.
Kwa upande wake Mwakilishi
mkazi wa Shirika hilo kwa upande wa Tanzania Dk.Beati Mboya alisema
lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ili kubaini mafanikio na
changamoto zinazovikabili vituo vinavyotekeleza mradi huo ilikuzipatia
ufumbuzi.
Alisema wanatarajia kufanya
tathmini hiyo kila baada ya miezi mitatu ili kuhakikisha hakuna
ucheleweshaji katika kutoa huduma baada ya kubaini changamoto na
kuzifanyia kazi kwa haraka.
Naye Kamanda wa Kikosi cha Afya
cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Paul
Kasabago alisema kikosi hicho kitaendelea kutoa huduma zilizobora ili
kuimarisha afya za Askari na familia zao kote nchini licha ya kukabiliwa
na upungufu wa wahudumu wa Afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni