Timu ya Taifa ya mchezo wa Roll yaenda Kenya
Meneja
Mauzo wa Kampuni ya Isere Sports inayouza vifaa vya michezo, Ismail
Bura (kulia) akionesha Kocha Mkuu wa mchezo wa Roll, Aurher Haule
sampuli ya sare za Taifa zinazofaa kuvaliwa na wachezaji wanapokuwa nje
ya nchi.
TIMU ya Taifa ya Mchezo wa mpira
wa kuteleza(Roll Ball) imeondoka jana ikiwa na wachezaji 12 kwenda Kenya
kwenye mashindano ya kimataifa ya Afrika yatakayoanza leo mjini
Nairobi.
Kocha Mkuu wa timu hiyo,Arthur
Haule alisema jana Dar es Salaam kuwa wamejiandaa kutwaa ubingwa wa
mchezo huo utakaoshirikisha timu kutoka mikoa sita.
Alisema safari yao ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Nadia House of Beuty inaondoka na wachezaji 12 na viongozi wawili.
Aliwataja wachezaji
watakaowakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Mohammed Athumani,
Emmanuel Thomas, Hamisi Salum, Rajab Kassim, Omari Madohola, Yakhe
Shaaban,Jonas Emmanuel, Fahadi Waziri, Said Abdallah,Kassim Rajab,
Feruzi Juma na Clement Andrea.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nadia
House of Beuty, Nadia Azmat akikabidhi vifaa vya michezo kwa safari hiyo
aliwataka watanzania wengine kusadia michezo ambayo haina umaarufu ili
kuibua vipaji mbalimbali vya vijana.
Nchi zinazoshiriki mashindanoi hayo ni wenyeji Kenya, Rwanda, Uganda, Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni