Wadau wa
Mawasiliano Kanda ya Ziwa, wakiwa katika picha ya pamoja katika Semina
juu ya utoaji wa elimu juu ya simu bandia (fake) na halali (orginal)
ulioandaliwa na TCRA, kabla ya kusitisha matumizi ya simu bandia mwezi
ujao.
Akizungumza kwenye semina ya wadau wa
mawasiliano wakiwemo wauzaji wa simu, Mafundi wa simu, wanahabari pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, Meneja
Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi, amesema takwimu za mpaka mwezi Machi mwaka
huu, zinaonesha kuwa asilimia tatu ya simu zinazotumika nchini ni bandia.
Amesema asilimia 13 ya simu zote
nchini ni zile zilizonakilishwa na kwamba idadi ya simu hizo zilizonakilishwa
imepungua kutoka asilimia 30 kutokana na elimu inayoendelea kutolewa na TCRA.
Ametanabaisha kwamba simu bandia zimekuwa
zikiingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa
wakitoa punguzo kubwa la bei kwa wateja wanaonunua simu hizo na hivyo
kuwahamasisha watu wengi kununua simu bandia.
Uchunguzi uliofanywa na TCRA umebaini
kuwa wastani wa bei ya simu halali kwa Tanzania ni kati ya shilingi elfu 20 hadi
elfu 60, bei ambayo wananchi wengi wanao uwezo wa kununua simu halali hivyo
waachane na matumizi ya simu bandia kwani zina madhara makubwa.
Kujua ikiwa simu yako ni halali,
unapaswa kutuma nambari za simu yako (IMEI Namba) kwenda 15090 ambapo utapokea
ujumbe mfupi wa maneno ukikujulisha ikiwa simu yako ni bandia (fake) ama halali
(Orginal) hii ikiwa ni bure kwa watumiaji wa mitandao yote.
Wadau wa Mawasiliano Kanda ya Ziwa,
wakiwa katika picha ya pamoja katika semina juu ya utoaji wa elimu juu
ya simu bandia (fake) na halali (orginal) ulioandaliwa na TCRA, kabla ya
kusitisha matumizi ya simu bandia mwezi ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni