MTOTO WA KITANZANIA ASHIRIKI KATIKA FILAMU YA KIMAREKANI
Tasnia ya filamu Tanzania inazidi kukua kwa kasi, si tu nyumbani hata nje ya nchi watanzania wanazidi kungara.
Safari hii mtoto wa watanzania
wenzetu aitwaye Evan Byarushengo amabahatika kupata nafasi ya kushiriki
katika filamu ya kimarekani iitwayo THE REAL MVP: The Wanda Durant
Story.
Filamu hii inajaribu kuonyesha
jinsi mama wa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant
alivyohangaika kuwakuza watoto wake mpaka kufikia kuwa mastaa. Evan
anaigiza kama Kevin Durant akiwa mtoto wa miaka 7. Waigizaji wakuu wa
filamu hii ni pamoja na Cassandra Freeman anayeigiza kama mama Evan;
Pauletta Washington (mke wake Denzel Washington) ambaye anaigiza kama
bibi
yake Evan na wengine wengi.
Juu, katika clip
mojawapo Evan akifanya mazoezi ya kucheza mpira wa kikapu. Nyuma ni
director wa filamu George Nelson na wasaidizi wake.
Juu, Evan akiwa anaongea na bibi yake (Pauletta) na mtoto anayeigiza kama kaka yake Kevin aitwaye Tony.
Juu Evan(aliyechuchumaa) akipitia script mbele ya wenzake.
Evan na mwenzake mwishoni walipata bahati ya kuonana na mama yake Kevin ambaye stori ya filamu inamuigiza.
Unaweza kuona clips za hiyo movie kupitia links hizi za youtube.
Kwa walio Marekani na Canada, movie hiyo itaonyeshwa siku ya Ijumaa na Jmosi kupitia Lifetime Channel 8/7c
Tuendelee
kumwombea mtanzania mwenzetu aende mbele zaidi ili tuzidi kuipeperusha
bendera yetu. Evan amefanya audition nyingi kwahiyo Mungu akipenda
ataonekana kwenye matangazo ya kibiashara na filamu zaidi.
Asante sana,
Dr. Philomena Ishengoma & Godfrey Byarushengo
Wazazi wa Evan
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni