MWENYEKITI WA MTAA WA BABALE ULIOPO WILAYA YA NYAMAGANA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WASIOFAHAMIKA WAKATI AKIELEKEA NYUMBANI KWAKE.
MNAMO TAREHE 22.05.2015 MAJIRA
YA SAA 20:00HRS KATIKA MTAA WA BULALE KATA YA BUHONGWA WILAYA YA
NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWENYEKITI WA MTAA WA BUBALE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALPHONCE MUSSA NYINZI MIAKA 48, MSUKUMA
MFANYABIASHARA NA MKAZI WA BULALE ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA
KUTOKEA CHINI YA KWAPA UPANDE WA KULIA NA WATU WAWILI WASIO FAHAMIKA.
RISASI HIYO PIA ILIMJERUHI NEEMA MARANGULA MIAKA 23 MKAZI WA BULALE
KATIKA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA.
INAELEZWA KWAMBA SIKU HIYO
JIONI ALIKUA AMETOKA KWENYE KIKAO ALICHOFANYA NA WAJUMBE WA KAMATI YA
ULINZI NA USALAMA WA MTAA WA BULALE, KATIKA MUDA WA SAA 20:00HRS USIKU
AKIELEKEA NYUMBANI AKIONGOZANA NA WAJUMBE WAWILI ALIKUTANA NA NEEMA
MARANGULA AKIWA NA MUME WAKE AMBAO WALIKUA WANAWAFUATA MAREHEMU NA
BALOZI KWA AJILI YA KUZUNGUMZIA MZOZO WA NDANI YA NDOA YAO KWA HIYO
WALIKUA WANAHITAJI KUSULUHISHWA, MAREHEMU NA WAJUMBE WAKE WAWILI WAKIWA
PAMOJA NA BI NEEMA PAMOJA NA MUMEWE WAKIWA WANAJADILI TATIZO HILO HAPO
BARABARANI MARA GHAFLA WAKATOKEA WATU WAWILI AMBAO WALIKUA WAKIPITA
BARABARANI NA KUWAAMBIA MKO CHINI YA ULINZI NA MMOJA WAO AKATOA BUNDUKI
NA KUMPIGA RISASI MAREHEMU AMBAYE ALIANGUKA CHINI HUKU WENZAKE
WAKIKIMBIA KUJIOKOA KUTOKA ENEO HILO LAKINI PIA WALE WAHALIFU
WAKAKIMBIA NA KUTOKOMEA GIZANI VICHAKANI.
NDIPO WANANCHI WA ENEO HILO
WALIJITOKEZA KWA MSAADA WA KUMSAIDIA MAREHEMU, WALIMCHUKUA MAREHEMU
KUMKIMBIZA HOSPITALI KWA MATIBABU LAKINI ALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI.
MAJERUHI BI NEEMA MARANGULA AMELAZWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU
TOURE KWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI. MWILI WA MAREHEMU UPO
HOSPITALI MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, UCHUNGUZI TUKIO HILO BADO
UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA JESHI LA POLISI AHMED MSANGI
ANAWAOMBA WANANCHI WENYE TAARIFA ZOZOTE KUHUSIANA NA TUKIO HILO
ZITAKAZO SAIDIA KUFANIKISHA KUKAMATA WAHUSIKA WAZITOE POLISI LAKINI PIA
KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WAO NA KUHAKIKISHA WANATENGENEZA MAKAZI
SALAMA HUKO WANAPOISHI NA MAENEO YA SHUGHULI ZAO. MSAKO MKALI UNAFANYIKA
NA KUHAKIKISHA WAHUSIKA WA TUKIO HILO WANAKAMATWA.
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni