WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KULAANI MAUAJI YA MTOTO SARA MGIMBA (14) WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO YALAANI MAUAJI YA MTOTO SARA MGIMBA (14)
Wizara imesikitishwa na taarifa
ya kifo cha mtoto Sara, ambaye mwilini wake ulioopolewa mtoni akiwa
alitobolewa macho, mwilini akiwa mtupu; jambo linaloashiria kuwa
marehemu alibakwa kabla ya mauti kumfika. Inaelezwa kuwa, alifungwa
kanga shingoni, na kufungiwa ndani ya sandarusi mbili (2) zenye mawe, na
kuzamishwa mto Lugarawa, hadi Uongozi wa kijiji cha Lugarawa walipoopoa
mwili wake majini wakati walipoendesha msako, mapema wiki hii.
Wizara inapongeza juhudi za
wanakijiji na jeshi la Polisi katika mkoa wa Njombe ambao walifika
sehemu ya tukio ili kufuatilia mauaji hayo. Ni imani ya Wizara ya watoto
kuwa, Polisi kwa kutumia weledi wao na kwa kushirikiana na wananchi
wataweza kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo na kuwachukulia hatua
stahiki.
Wizara inasisitiza kwamba kila
binadamu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kwa
mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya ubakaji na maujai ya kikatili
vinapotokea katika familia zetu vinadhohofisha juhudi za wananchi katika
kujiletea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi, hivyo ni muhimu kuzuia
na kutokomeza aina zote za ukatili kwa watoto.
Wizara inaomba wanafamilia
waliopatwa na msiba huu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha
majonzi makubwa, wakati Polisi wakiendelea kuwasaka watuhumiwa wa mauaji
hayo.
Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
15/4/2016
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni