ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA.
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada yakujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio
 hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia 
kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na 
kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.
Mashuhuda
 wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema 
huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha 
ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na 
kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa 
akiyatumia.
Akizungumza
 kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, 
mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni 
yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa 
hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.
Baadhi
 ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana
 huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu “rukaa,
 ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume” hali ambayo ilikuwa 
ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati
 ya mnara huo.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni