| MBUNGE wa  jimbo la  Iramba 
wilayani Iramba mkoani Singida Bw Mwigulu Nchemba  ameendelea  kufanya 
mikutano ya  kuwashukuru  wananchi  wake  kwa  kumchagua  kwa  kishindo 
 katika  uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa  kutekeleza ahadi  mbali mbali  
alizopata kuwaahidi  wakati wa kampeni .
 
 Mbunge Nchemba  amekabidhi  
bati  hizo  jana  wakati wa mikutano yake ya  kuwashukuru  wananchi wake
 wa  jimbo la Iramba kwa kumchagua na kuanza utekelezaji wa ahadi  zake.
 Alisema   kuwa  lengo la  
kuanza  kukabidhi ahadi  zake ni  kuwafanya wananchi kuharakisha  
ukamilishaji wa  shughuli za kimaendeleo jimboni hasa katika nyanja ya  
elimu  na afya  na kuwa  bati  hizo  zitasaidia  ujenzi wa vyumba  vya  
madarasa ,nyumba za  walimu na  Zahanati  .
 Kwani  alisema ndoto  yake ya 
mbeleni   ni kuona jimbo la Iramba na  wilaya ya Iramba  inaendelea  
kuwa mbele katika ubora wa vyumba  vya madarasa na  wengine  kufika  
kujifunza Iramba
 Hivyo  alisema pamoja na  
kuchangia  bati  kwa  ajili ya ujenzi  huo bado atajitolea  kununua  
tofari  za  kujengea ambazo kwa  kila kijiji  vijana  watafyatua na yeye
 atazinunua kwa  bei ambayo  wao  watataka  kama  sehemu ya  kutoa ajira
 kwa vijana  vijijini pia vifaa vyote  vya  viwandani kwa ajili ya 
ujenzi wa miradi hiyo  ni juu yake wananchi wanachotakiwa kufanya ni  
kushiriki katika shughuli za  kimaendeleo .
 Pia  aliwataka  walimu na  
watumishi  wanaopangwa  kufanya kazi katika  wilaya  ya  Iramba  
kujenga  utamaduni wa kupenda  kufanya kazi katika wilaya  hiyo  badala 
ya  kuripoti na kuondoka .
 Nchemba ambae ni waziri wa  
kilimo ,mifugo na uvuvi  alisema  kuwa vipaumbele  vyake  kwa  wananchi 
wake ni maji na umeme ambavyo tayari umeme  umeanza  kusambazwa  
vijijini  pia maji anaendelea  jitihada japo  alisema suala la 
Miundombinu bado ni  changamoto .
 Wakati  huo  huo waziri Nchemba
 ameshauri  uongozi wa Halmashauri  kuruhusu  wanafunzi wanaopata 
matatizo ya ugonjwa wakiwa shuleni  kupatiwa matibabu ya  bure katika  
vituo  vya afya ,Hospitali na zahanati katika  jimbo  hilo  badala ya  
kuwarudisha  nyumbani .
 Alisema kuna haja ya 
Halmashauri  kupitia  vyanvzo  vyake  vya ndani  kusaidia  kuwalipia 
matibabu   wanafunzi hao na kuwa  ofisi yake  itasaidia   kufidia pesa  
hizo kwa  kugharamia baadhi ya  miradi ambayo inapaswa  kutekelezwa na 
Halmashauri kama ambavyo anafanya sasa kwa kujitolea kujenga vyumba vya 
madarasa na  Zahanati .
 | 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni