HIZI NI SABABU ZA AZAM KUPOKWA POINTI TATU
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), limepitia marejeo ya uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania Bara (TPLB) kuipoka pointi zake ilizovuna kutoka mchezo Na.
156 dhidi ya Mbeya City ya Mbeya katka mchezo uliofanyika Uwanja wa
sokoine mjini Mbeya.
Katika
Kamati Maalumu ya TFF iliyoketi ndani ya saa 72, chini ya sekretarieti
ya TFF na Bodi ya Ligi, iliyoketi Mei 17, 2016 iliipokea marejeo
(revision letter) ya Azam kuhusu kupokwa pointi hizo iliamua kuingiza
suala la Azam kama ajenda na kuangalia sababu za bodi kufikia uamuzi
huo.
Kamati
ilibaini kuwa mchezaji Erasto Nyoni alikuwa na kadi tatu za njano
ambazo ya kwanza aliionywa katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young
Africans uliofanyika Agosti 22, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kadhalika
kamati ilibaini mchezaji huyo wa Azam FC alionyeshwa tena kwa mara ya
pili katika mchezo Na. 4 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya
Tanzania Prisons uliofanyika Septemba 12, 2015 kwenye Uwanja wa Azam
Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia,
Nyoni wa Azam FC alionywa tena kwa kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya
Coastal Union ya Tanga katika mchezo Na. 152 uliofanyika Mkwakwani mjini
Tanga, uliofanyika Februari 14, 2016 hivyo ilibidi mchezaji huyo
asimame mchezo Na. 156 wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, uliofanyika
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, lakini alichezeshwa na ndipo adhabu
inapoiangukia Azam.
Mchezo
Ngao ya Jamii unahusishwa kwa sababu za kanuni 16 (7) ya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara, inayosema: “Vitendo vya utovu wa nidhamu na
ukiukwaji mwingine wa taratibu za mchezo katika mchezo wa Ngao ya Jamii
utachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni hizi ambapo uamuzi wowote dhidi
yake utakuwa na uhusiani wa moja kwa moja na Ligi Kiu, na mechi za ligi
zinazohusisha timu husika.”
Katika
kutafuta marejeo ya adhabu hiyo, Azam waliiandikia barua TFF wakisema
mchezaji huyo alimaliza adhabu yake kwa kutocheza mchezo dhidi ya Yanga,
Dar es Salaam kabla ya kwenda Mbeya na hivyo Erasto hakuwa na adhabu
hiyo ambayo imeigharimu timu hiyo.
Awali
TPLB iliinyang’anya ushindi wa Azam ambao ulikuwa ni wa pointi tatu na
mabao matatu uliyovuna dhidi ya Mbeya City kutokana na kumtumia mchezaji
Erasto Nyoni kwenye mechi hiyo wakati akiwa na kadi tatu za njano. Azam
walipinga hatua hiyo.
TPBL
ilifanya uamuzi huo, kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo
la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao
matatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni