CHUMBA CHA DEREVA TAX CHAZUA KIZAA ZAA MTAA WA MBEZI MTONI GOLD STAR, DAR
Wananchi na mwenye nyumba wakifungua mlango
Chupa zinazodaiwa kuwa na mikojo zikiwa zimetapakaa ndani ya chumba hicho.
Huyu Ndiye Dereva wa Tax Nyati anayedaiwa kumiliki chumba hicho.
UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba
 cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga 
pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata 
bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold 
Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
Mtandao huu ulipata fursa ya 
kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya wakazi wa 
mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku na 
sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo
 aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama ‘NYATI’.
Akizungumza na mtandao huu wa 
Sufianimafoto, Mama mwenye nyumba kuhusu tukio hilo, alisema kuwa siku 
ya Mei 23, akiwa ameketi uwanji karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo 
huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma 
kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu 
mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho kupitia 
chini ya mlango.
Kesho yake Mei 24 Baada ya kuona 
wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita jirani yake na 
kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa na 
mashaka na chumba hicho.
Mei 25 Mama mwenye nyumba aliamua
 kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili Makoye, kutoa taarifa juu ya 
wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na kuongozana na Viongozi wengine,
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine 
 Abdalla Mlaliya na Matrida Paston, waliofika na kujionea hali halisi ya
 chumba hicho.
Baada ya viongozi hao kufika 
eneola tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo 
cha Polisi.  Mama huyo alitekeleza agizo na kwenda kuripoti Kituo cha 
Mbezi Garden na kuongozana na Mkuu wa Kituo hicho na baadhi ya askari 
hadi nyumbani na kukuta hali hiyo ya sintofahamu.
Walipofika eneo la tukio na 
kushuhudia hali hiyo, Mkuu wa Kituo aliamuru mlango huo uvunjwe huku 
wanachi na Viongozi wa Mtaa huo wakishuhudia na kuingia ndani ambako 
walikuta Chumba kizima kikiwa kimejaa Chupa za Plastiki zilizojaa 
mikojo, Mifuko ya Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja iliyochomekwa kwenye
 Soketi ya Umeme ukutani, Pakiti nyingi tupu za Sigara aina ya Embassy 
na Kondomu zilizotumika na zisizotumika.
Baada ya zoezi hilo, Mwenyenyumba
 alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka kurejea nyumbani, lakini Dereva
 huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa mbali maeneo ya Kunduchi na 
kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.
Hadi Mtandao huu unaondoka eneo 
la tukio majira ya saa tano usiku bado wakazi wa maeneo hayo walikuwa 
wamejazana nje ya Chumba hicho wakiendelea kumsubiri arudi ili kupata 
ukweli kuhusu mambo waliyoyaona katika chumba chake.
Aidha Mama mwenye nyumba 
aliuambia mtandao huu kuwa mpangaji wake huyo, tangu alipohamia katika 
nyumba hiyo mwaka 2008, hakuwahi kumuona akiingia na mwanamke katika 
chumba hicho, wala kumuona mgeni wa aina yeyote kwa Dereva huyo,jambo 
lililomshangaza kukuta Kondom zilizotumika katika chumba hicho. Ama 
kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauun.
Hadi leo hii Mei 27, mtandao huu 
umeshindwa kumpata dereva huyo baada ya kutompata hewani simu yake ikiwa
 imezimwa tangu kutokea kwa tukio hilo.  
Leo hii Mei 27, Mama mwenye 
nyumba ameripoti kuwa mpangaji wake huyo,hajatokea nyumbani hapo tangu 
kutokea kwa tukio hilo ambapo leo, amechukua uamuzi wakuwalipa vijana wa
 mtaa huo ili wasafishe chumba hicho.
Tayari tumewalipa pesa vijana kiasi cha sh.200,000/= ili wafanya usafi na wameshamaliza na kwenda kufukia bonde la mto Mbezi.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni