TRA YAWAPA ELIMU YA MLIPAKODI WAFANYABIASHARA RAIA WA CHINA WAISHIO NCHINI TANZANIA
Meneja
 wa Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Bi. Diana Masalla akitoa elimu ya 
mlipa kodi na sheria za kodi  kwa wafanyabiashara raia wa China 
wanaoishi hapa nchini na kufanya biashara katika semina ya mlipa kodi 
iliyofanyika leo kwenye mgahawa  wa Tang Ren Chinese jijini Dar es 
salaam,   ambapo kabla  semina hiyo  imefunguliwa na Bw. Sun Chengfeng 
Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibiashara kutoka serikali ya Watu 
wa China nchini Tanzania, Semina hiyo inalenga kuwapa wafanyabiashara 
hao elimu na uelewa wa masuala mbalimbali  ya kisheria katika kodi na 
umuhimu wa  kulipa kodi.
Baadhi
 ya wafanyabiashara raia wa China wanaoishi  nchini Tanzania na kufanya 
biashara wakiwa katika semina ya mlipa kodi iliyofanyika leo kwenye 
mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam
Bw.
 Sun Chengfeng Mwakilishi wa masuala ya Kiuchumi na Kibashara kutoka 
Serikali ya Watu wa China nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi
 wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo  iliyofanyika kwenye 
mgahawa wa Tang Ren Chinese jijini Dar es salaam.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni