WIZARA YA KUDHIBITI MIGOGORO YA ARDHI KWA KUFUNGUA MABARAZA YA ARDHI
Jengo la Baraza la Ardhi Kiteto.
…………………………………………………………………………………………..
Katika azma ya kuimarisha huduma
ya utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imeendelea kuboresha na kufungua Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya yatakayohusika na migogoro katika maeneo mbalimbali
nchini.
Kwa upande wa Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya mapya, Baraza ambalo limeshaanzishwa rasmi, ni lile
lililopo katika wilaya za Kahama na tayari limepatiwa vitendea kazi
muhimu na watumishi.
Wizara imeunda Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya wilaya mapya 47 kupitia GN 544/2016, kati ya mabaraza hayo
mapya 47, Mabaraza ya Lushoto, Kiteto, Kasulu, Kibondo na Bagamoyo
yamepatiwa vitendea kazi na yataanza kufanya kazi mwishoni mwa mwaka huu
wa fedha.
Aidha, uimarishaji wa Mabaraza
hayo utapunguza mlundikano wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na
Nyumba ya Wilaya kwa kuwa migogoro isiyo ya lazima kwenda ngazi ya
wilaya itasuluhishwa katika ngazi ya kijji au kata.
Katika picha ni baadhi tu ya
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ambayo yapo tayari kufunguliwa;
Kiteto, Lushoto, Kigoma mjini na Kibondo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni