KONGAMANO LA WADAU WA VITAMBULISHO NIDA LAFANYIKA (BOT) DAR ES SALAAM
Naibu
Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akifungua kongamano la wadau kuhusu
vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika ukumbi wa Benki Kuu na
kuhudhuriwa na wadau toka sekta mbalimbali nchini
Mkurugenzi
mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust Sosthenes Kewe akichangia
mada wakati wa kongamano wa wadau lililohusu mpango wa Usajili
vitambulisho vya Taifa
Mr.
Sanjay C. Rughani Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA)
na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini akiwasilisha mada
wakati wa kongamano la wadau katika mpango wa usajili vitambulisho vya
Taifa
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dkt. Modestus
Kipilimba akionyesha wadau sampuli ya vitambulisho vyenye saini
vitakavyoanza kutolewa hivi karibuni, wakati wa kongamano la wadau
kuhusu mpango wa vitambulisho vya Taifa
Baadhi
wa washiriki wa Kongamano la wadau kuhusu mpango wa Usajili
vitambulisho vya Taifa wakisikiliza kwa makini mada ya mkakati wa
Usajili kufikia Disemba 31,2016 iliyowasilishwa na NIDA
……………………………………………………………………………………………………….
Na Rose Mdami
Wadau kutoka Sekta mbalimbali
nchini leo wamekutana katika kongamano maalumu kujadili suala la
Vitambulisho vya Taifa na uwezekano wa kukamilika kwa mradi huo ili
kuwezesha taifa kuwa na Kanzidata(database) yenye taarifa sahihi zenye
kujibu maswali makuu nini ni nani, yuko wapi na anafanya nini. Lengo ni
kurahisha utoaji huduma na kuwezesha wananchi kujishughulisha na masuala
ya biashara kwa kuwa na mfumo rasmi unaowatambua
Akifungua kongamano hilo, Kaimu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Nato Mwamba amesema mfumo wa
Usajili na Utambuzi wa Watu ni mfumo ambao umesubiriwa kwa siku nyingi
kwani manufaa yake ni makubwa katika mifumo mbalimbali nchini hususani
mfumo wa biashara na taasisi za fedha nchini
Amesema kutokana na kupanuka kwa
matumizi ya teknolojia nchini, huduma nyingi zikiwemo huduma za kifedha
zinategemea sana kuwepo kwa mfumo wa Vitambulisho vya Taifa ili
kuwezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma zitolewazo kwa sasa kwani
wengi wanakwama kwa kuwa hakuna mfumo rasmi unaowatambua. Mafanikio ya
mfumo huu ni kufungua milango kwa wananchi wengi zaidi kunufaika na
huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa nchini zikiwemo huduma za
kifedha na hivyo kuwataka wadau hao kuwezesha NIDA kufikia malengo ya
usajili nchi nzima kufikia Disemba 31, 2016 ili mfumo wa Utambuzi wa
Taifa uweze kuunganishwa na mifumo mingine
Akieleza mkakati wa usajili
kufikia Disemba 31, 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Medestus
Kipilimba amesema NIDA imejizatiti kutumia taarifa za zilizokusanywa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanza usajili utakaowezesha wananchi
waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura kuhakikiwa na kupata usajili
awamu ya kwanza ambao utahusisha namba ya utambulisho kabla ya kupata
kitambulisho cha Taifa. Amesema hatua ya kufanya usajili wa awali na
kutoa namba ya utambulisho itawezesha wananchi kuanza kufaidi
utambulisho wao kwa kuwawezesha kupata huduma mbalimbali. Hata hivyo ili
mwananchi kupata utambulisho kamili lazima kukamilisha hatua za usajili
kwa kuhakikisha anawasilisha nyaraka muhimu za utambuzi ili kuendelea
kupata huduma nyingine
Kwa mara ya kwanza NIDA itaanza
kuzalisha vitambulisho vyenye saini ya mwombaji ambayo itawekwa kwenye
uso wa mbele wa kitambulisho na nyumba ya kitambulisho kutakuwa na saini
ya mtoaji. Amesema hatua zote katika kukamilisha mpango huo
zimekamilika
Kongamano hilo limehudhuriwa na
wadau toka Taasisi za fedha nchini, TASAF, Wamiliki wa makampuni ya simu
nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Benki ya Dunia (World Bank),
SSRA, BIMA, Melinda and Bill Gates Foundation, Tanzania Bankers
Association( TBA) na wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Serikali
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni