BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPITISHWA, USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA TANZANIA WAPIGWA MARUFUKU KWA MIAKA 3.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne akijibu hoja na michango
mbalimbali ya wabunge zilizoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa
Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka
2016/2017
ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Baadhi
ya wabunge wakimpongeza wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe
mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo
imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akimweleza jambo Mbunge
wa Bunda mjini Mhe. Esther Matiku (CHADEMA) nje ya ukumbi wa Bunge mara
baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi
ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.
ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni
mjini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dodoma.
Serikali imesimamisha utoaji wa
vibali na uuzaji wa wanyama hai kutoka katika hifadhi za Taifa kwenda
nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge iliyoelekezwa kwenye
wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi
bilioni 135.7.
Prof. Maghembe ameiagiza Idara ya
Wanyamapori ipange na kuweka utaratibu mpya utakaotumika kusimamia
biashara hiyo pindi itakaporejeshwa tena baada ya kumalizika kwa muda wa
zuio la Serikali la miaka 3 ikizingatia mazingira ya uhifadhi wa
wanyama hao.
USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA NCHI.
Amesema kumekuwa na taarifa za
baadhi ya watanzania wasio waaminifu ambao wamekua wakijihusisha na
vitendo vya kusafirisha wanyama hai waliokatazwa kinyume cha utaratibu
jambo ambalo limeisababishia Serikali ipoteze mapato kutokana na wanyama
hao.
Kuhusu wanyama wanaoruhusiwa
kusafirishwa kama nyani, Kenge,ndege, kobe, wadudu na tumbili amesema
kuwa wamekuwa wakisafirishwa kinyume na utaratibu na baadhi ya
wafanyabiashara wasio waaminifu kwa ajili ya kutumiwa na makampuni ya
kimataifa kwenye shughuli za utafiti wa kisayansi wa tiba na chanjo.
Amesema makampuni hayo yamekuwa
yakinufaika binafsi kwa kupata fedha nyingi pindi yanapofanikiwa kupata
chanjo au tiba husika huku maeneo waliokotoka yakipata fedha kidogo
jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imeamua kulifanyia kazi.
UTALII KUSINI MWA TANZANIA NA MAENEO MENGINE.
Amesema Serikali itatekeleza
miradi mbalimbali ya uboreshaji wa Utalii wa Kusini ili kuweka mazingira
wezeshi na kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikisababisha watalii kushindwa
kufika katika maeneo ya hifadhi za Taifa eneo la ukanda wa kusini mwa
Tanzania.
Baadhi ya maeneo
yatakayoshughulikiwa ni gharama ya usafiri wa ndege kwenda na kurudi
katika maeneo hayo kuwa kubwa hadi kufikia Dola za kimarekani 1800 jambo
ambalo limekuwa kikwazo kwa watalii hao.
Amesema Serikali itaanzisha vituo
vya kuwekea mafuta ya ndege mahali vilipo vivutio vya utalii ili
kuziwezesha ndege ndogo kufika kwa urahisi na kupata huduma ya kuongeza
mafuta ili kupunguza gharama kwa wasafiri wanaotembelea hifadhi za eneo
hilo.
Aidha amesema katika mwaka wa
fedha 2016/2017 Serikali itanunua ndege ndogo abiria ili kuwezeha
watalii kufika kwa urahisi katika maeneo ya hifadhiza Taifa.
UTAMBUZI WA MAENEO MAPYA YA UTALII.
Serikali kwa kushirikiana na
Wakuu wa wilaya, mikoa na Wabunge itaanzisha mpango mpya kuviorodhesha
vivutio vyote vya utalii vilivyo katika maeneo yao ili viweze kutangazwa
ipasavyo na kuongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mpango huo
itaandaliwa orodha ya vivutio hivyo ili vianzwe kutangazwa rasmi.
Katika kuimarisha shughuli za
utalii nchini serikali itaweka mkazo katika uimarishaji wa utalii wa
utamaduni, uimarishaji wa maeneo ya historia na Malikale ili kuwezesha
eneo hilo kuchangia zaidi katika pato la taifa.
ULINZI NA USALAMA WA HIFADHI ZA TAIFA.
Prof. Maghembe ameeleza kuwa
suala la ulinzi na usalama wa hifadhi zote za Taifa liko kwa mujibu wa
sheria na kubainisha kuwa serikali imeanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania(TAWA) litakalochukua mbuga zote zilizokuwa na
uongozi ambazo ziko nje ya TANAPA.
Jeshi hilo litapambana
kikamilifu na ujangili, kuimarisha maadili na nidhamu ya askari wa
ulinzi wa hifadhi za taifa pamoja na kushughulikia maslahi yao na
kuondoa migogoro kati ya askari na wananchi.
Amesisitiza kuwa mara baada ya
Bunge la Bajeti, Wizara itakutana na wahifadhi wakuu wote ili kuweka
vigezo vya kuzingatia katika majukumu yao na kusisitiza kuwa wahifadhi
wote watakaoshindwa kwenda na kasi ya vigezo vilivyowekwa
hawatajumuishwa kwenye jeshi hilo.
Aidha, amekemea vikali vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi kupiga raia na kuchoma
nyumba za wananchi kuwa havikubaliki na ni kinyume cha majukumu yao.
” Nimesikiliza kwa makini
michango ya wabunge na nimesikia wafanyakazi katika hifadhi zetu
wanapiga raia wanaua mifugo na kuchoma nyumba za wananchi jambo ambalo
halikubaliki, hatukuwatuma kufanya hivyo” Amesisitiza Prof.Maghembe.
MIGOGORO YA MIPAKA MAENEO YA HIFADHI.
Serikali imesema mpaka sasa kuna
migogoro ya ardhi 281, kati ya hiyo 35 ambayo ni sawa na asilimia 12.5
ni migogoro ya hifadhi na kuita Mikoa yenye migogoro hiyo kuwa ni
pamoja na Mara , Tanga na Kagera inachukua jumla ya asilimia 50.
Aidha, amesema kuwa mkoa wa
Tabora unaongoza kwa kuwa na eneo kubwa la ardhi na unaongoza kwa kuwa
na migogoro mingi ya hifadhi kwa asilimia 40.
Katika kuishughulikia migogoro
hiyo Serikali imeziagiza wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Maji na Umwagiliaji, TAMISEMI, Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa
Rais – Mazingira pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana
pamoja katika kutatua migogoro yote ya ardhi nchini.
UBORESHAJI WA MAENEO YA HIFADHI NA MAMLAKA ZA UHIFADHI.
Amesema katika mwaka wa fedha wa
2016/2017 kiasi cha shilingi bilioni 1 kimetengwa kushughulikia usafi
wa mazingira na ujenzi wa vyoo vya kisasa katika hifadhi ya mlima
Kilimanjaro vitakavyokuwa na uwezo wa kugeuza maji taka kuwa poda ili
kuweka mazingira yote ya mlima huo kuwa safi.
Aidha,amesema kuwa Mamlaka za
hifadhi za Taifa zimeendelea kuchangia katika maendeleo ya wananchi
katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa madarasa, miundombinu
ya barabara, utoaji wa madawati katika halmashauri mbalimbali nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni