Tigo yatoa kompyuta 20 zilizounganishwa na intaneti kwa sekondari 3 Mtwara
| Wanafunzi wakishuhudia makabidhiano hayo | 
 Kampuni
 inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania leo imetoa 
kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 33 zikiwa na huduma ya 
bure ya intaneti iliyogharimu 22m/- kwa shule  tatu za sekondari mkoani
Mtwara. Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
Mtwara. Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
Akizungumza
 wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika Shule ya Sekondari Sino 
mkoani Mtwara Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles 
alisema, “Msaada huu kwa shule hizi tatu ni sehemu ya
mkakati wa kampuni wa kuleta mageuzi katika mtindo wa maisha ya kidijitali. Msaada huu wa leo umekuja baada ya kukabidhi kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Chuda mkoani Tanga na kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti kwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure mkoani Mwanza mwaka jana.

“Msaada
 kwa shule ya Sekondari ya Masasi, Tandahimba na Sino ni kielelezo cha 
kweli cha uwekezaji wa Tigo katika miradi tofauti yenye mchango kijamii 
kupitia mkakati wetu wa kuwekeza kijamii unaowezesha jamii kupokea zana 
za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katikanyanja zote za 
kijamii ikiwemo sekta ya elimu,” alisema Charles.
Tukio
 hilo ambalo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego 
ambaye alizitaka sekta binafsi kuisaidia serikali katika mikakati yake 
katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zilizopo nchini.
Dendego
 alisema, “Naipongeza Tigo  kwa ukarimu wao wa kuzisaidia shule hizi 
natoa wito kwa watu binafsi kampuni za biashara na wadau wengine 
kujitokeza katika kuunga mkono juhudi za kuboresha
sekta ya elimu.”
sekta ya elimu.”
Akipokea
 msaada huo kwa niaba ya wakuu wenzake wa shule za sekondari, Mkuu wa 
Shule ya Sekondari Sino Riyadh Kadhi alisema kwamba kompyuta hizo 
zitawawezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa kiteknolojia na kuwawezesha 
 kuipata teknolojia ya habari mapema katika elimu yao. “Tunafurahi kwa 
hatua hii ya Tigo; tuna
matumaini kwamba kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa ujumla,” alisema Kadhi.
matumaini kwamba kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa ujumla,” alisema Kadhi.
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni