Maliasili na Tamisemi wasaini mkataba wa makubaliano uendelezaji misitu
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo
Wizara
ya maliasili na utalii kupitia wakala wa huduma za misitu leo wamesaini
mkataba wa makubaliano kuhusu ushirikiano wa uendelezaji misitu na
wizara ya TAMISEMI.
Maeneo ya kuzingatia
katika mkataba huo yametajwa kuwa ni kuimarisha ushirikiano katika
Misitu na utawala bora, uperembaji miradi inayofadhiliwa na mfuko wa
misitu Tanzania pamoja na kuboresha ukusanyaji, ugawaji, utumiaji na
ufuatiliaji wa matumizi ya asilimia 5 ya tuzo za upandaji miti.
Awali kabla ya kusaini
mkataba wa makubaliano katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi alisema wizara yake inalenga kuimarisha
utendaji wake hivyo aliwaagiza watendaji kusimamia misingi ya mkataba
huo wa makubaliano katika utekelezaji wa majukumu ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu TAMISEMI Injinia Musa Iyombe ambaye amewakilishwa na Bw. Mohamed
Pagawa aliwataka Maafisa Misitu kufanya kazi kwa ushirikiano kama
Mkataba Unavyotaka lakini pia kuzingatia sheria, kanuni na Utaratibu
katika uendelezaji wa Rasilimali Misitu
Mkurugenzi wa Mipango
na Matumizi ya Rasilimali Misitu Bw. Mohamed Kilongo akitoa ufafanuzi
kuhusu makubaliano hayo amesema tathmini ya Rasilimali Misitu
inakabiliwa na changamoto kuu mbili na amezitaja kuwa ni uharibifu
Mkubwa wa Misitu unaofikia kiasi cha hekta 372,000 kwa mwaka na mahitaji
ya mazao ya misitu kwa mwaka yanazidi uwezo wa Misitu kwa zaidi ya Meta
za ujazo Milioni 19.5.
Amesema ili kukabiliana
na changamoto hizo kunahitajika jitihada za pamoja kuboresha usimamizi
wa rasilimali za misitu na kupunguza uharibifu katika hifadhi zetu. Kazi
kubwa iliyopo mbele yetu ni kupanda miti hekta 185,000/= kwa mwaka kwa
ajili ya kukidhi mahitaji ya Mazao ya Misitu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni