Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vyazidi kupungua Nchini.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na
Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo
pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho
ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari
na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika
Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza
rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni
10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
Mshauri
wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia
na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya
Taifa jijini Dar es salaam.
Wadau
mbalimbali wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt.
Margaret Mbando hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha
yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es
salaam.
Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .
Akizungumza hayo katika hafla
fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto , Mkurugenzi wa Tiba Dkt.
Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kufikia
malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na
wakina mama.
“Tumefanikiwa kupunguza Idadi ya
vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia malengo ya milenia
kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima ya afya kwa jamii”
alisema Dkt. Mbando.
Mbali na hayo Dkt Mbando amesema
kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani wakazi wa Dar es salaam
kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo yenye kauli mbiu ya “Huduma
Bora kwa Afya Bora”yatayofikia kilele mpaka Juni 10 mwaka huu ili kupata
ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa jijini.
Aidha ameipongeza Serikali ya
Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana vizuri na Serikali ya
Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro milioni 47 kwa muda wa
miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.
Kwa upande wa balozi wa Ujerumani
Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango wa Serikali ya ujerumani kwa
sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa sehemu ya mpango wa ushirikiano
wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni