BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO
 Baadhi
 ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya 
ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha 
maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya 
Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma.
 Naibu
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter 
Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi 
Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge.
 Naibu
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter 
Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma
 nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. 
 Mwanasheria
 Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi 
wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea 
Bunge mjini Dodoma. 
 akiwasisitiza
 jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) 
alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
 Waziri
 wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) 
akimweleza jambo Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi 
(MoCU) Bw. Frank Nkya (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
 Waziri wa Elimu,Sayansi
 na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kulia)akijadiliana jambo 
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. 
Angella Kairuki (kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na 
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni