|  | 
| 
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiongea na waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa  huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games jijini Dar Es Salaam jana.Tigo
 Games ni huduma katika wavuti  ambayo imesheheni  michezo mingi kwa 
ajili ya wateja wa Tigo wenye simu za Smartphone au Tablet zinazotumia 
mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakua App ya 
Tigo Games. | 
|  | 
| Wasanii wakiigiza kama Mazombie katika kunogesha uzinduzi wa TIGO GAMES | 
|  | 
| Wasanii wakicheza mpira katika uzinduziwa tigo games mapema jana katika ukumbi wa High Spirit Jijini Dar es salaam | 
|  | 
| Wadau mbalimbaliwakipata taswira mbele ya gari katika RED carpert | 
|  | 
| Wasanii wakiwa katika pozi na mfano wa Risasi katika uzinduzi wa TIGO GAMES | 
|  | 
| Wadau wakifurahi jambo katika uzinduzi huo | 
|  | 
| Mtangazaji
 wa Choice Fm na Mchekeshaji Idris Sultan akiwa live jukwaani 
kusherehesha uzinduzi wa Tigo Games mapema jana katika ukumbi wa High 
spirit Jijini Dar es Salaam | 
|  | 
| Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akifurahi jambo na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) wakati wa uzinduzi | 
|  | 
| Wasanii wakitumbuiza nyimbo za michael Jackson | 
|  | 
| Mfanyakazi wa Huawei akielekeza jinsi ya kucheza Games hizo mbalimbali zinazopatikana katika Tigo Games | 
|  | 
| Baadhi ya wadau wakipata maelekezo jinsi ya kuingia katika mashindano ya kucheza Games na mshindi kujishindia Zawadi | 
|  | 
| Waadndishi wa habari wakishindana kucheza Games katika uzinduzi wa Tigo Games jana usiku | 
|  | 
| Msanii wa kizazi kipya Benpol akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa clouds tv Perfect baada ya uzinduzi wa tigo games | 
|  | 
| Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Tigo Games mapema jana usiku | 
|  | 
| Wadau wakipata picha katika sanamu za michezo ya Tigo Games | 
|  | 
| Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Tigo Games | 
 Kampuni ya simu inayoendesha maisha ya kidijitali Tanzania, Tigo, leo imetangaza uzinduzi wa huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo
 kama Tigo Games. Tigo Games ni huduma katika wavuti  ambayo imesheheni 
 michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenyeSmartphone au tablet 
zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakua App ya Tigo Games.
 Kwa
 wateja wenye simu za kawaida zilizo na intaneti watapata huduma hii 
katika tovuti ya Tigo Games.  Michezo zaidi ya 800,inapatikana kupitia 
huduma hii ikiwemo michezo maarufu ambayo ni pamoja na Buddy Man, Cut the Robe, Zombie Run na Tokyo Drift.
 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Huduma hii mpya ya michezo  inaifanya Tigo kuwa ya kwanza katikamitandao ya
 simu Tanzania  kutoa jukwaa la michezo linaloweza kutumiwa  na watu 
wengi ambapo wateja wa Tig0  wanaweza kucheza michezo mbalimbali 
 kulingana na chaguo lao kwa gharama wanayoimudu. 
Tigo imejikita kuendelea kusimamia maslahi ya wateja wake kwa kutoa  bidhaa nyingine nyingi  kwa ajili ya manufaa ya kuwa na simu za kisasa.” 
 “Tigo sasa ndio inaongoza katika upatikanaji wa huduma ya 4G LTE 
nchini, na kwa sasa huduma hii inapatikana katika miji mikubwa 12. Tunaamini
 kwamba wateja wetu watafaidika sana kutokana na intaneti yenye kasi 
zaidi itakayo wawezesha kupakua na kucheza michezo hii,” alisema 
Gutierrez.
Tigo Games ni huduma ambayo mteja akichajua kulipia mara moja, ataweza kuchagua michezoaipendayo na kuicheza atakavyo wakati wowote.  Kuna VIP Club ambayo inampa mteja uamuzi wa kujiunga na kifurushi cha siku, wiki na hata mwezi; pia kinamruhusu mteja kupakua michezo bila kikomo.
Mteja ataweza kucheza michezo kwa mda wowote autakao bila makato yeyote. Malipo
 ya utumiaji wa data kadri mteja anaendelea kucheza ndio yatakayo 
hitajika. Uzinduzi wa VIP Games Club utakapofanyika, siku 7 za mwanzo 
wateja wataweza kufurahia huduma bure kwa kutembelea wovuti huu: http://burudani.tigo.co.tz/games. 
“Kuanzishwa
 kwa bidhaa hii  kupo kwenye mikakati ya Tigo  ya kuwapatia wateja wake 
 bidhaa na huduma zilizo na ubora duniani  ambazo  zinawawezesha  
kufurahia kwa ujumla maisha ya  kidijitali,” alisema Gutierrez.
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni