Mshindi wa bahati nasibu ya Taifa kupatikana kesho
Mbunge
wa zamani jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa (kulia) akipewa maelezo namna
mshindi wa bahati nasibu ya Taifa atakavyopatikana mara baada ya kukata
tiketi ya mchezo huo katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma
jana baada ya kuzinduliwa rasmi ukataji tiketi za mchezo.
Wakala
wa ukataji tiketi za mchezo wa bahati nasibu ya Taifa mjini Dodoma
Jamila Baduwel akitoa huduma hiyo kwa mmoja wa wananchi aliyetaka
kununua tiketi za kushiriki.
…………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Baada
ya kampuni ya Murhandizwa kutoka nchini Afrika ya Kusini ambayo
ilipewa leseni ya kuendesha mchezo wa bahati nasibu ya taifa kuanza
kuuza tiketi za mchezo huo wiki iliyopita ,leo (Jumamosi) ndio mchezo wa
kwanza utafanyika na mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100
atatangazwa.
Mwenyekiti
wa kampuni ya Gidani International ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya
Murhandizwa,Prof .Bhongani Khumalo alisema kuwa michezo yote
itaendeshwa kwa utaalamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kwa uwazi
vilevile kuanza kwa mchezo huo hapa nchini ni mwendelezo wa michezo
mingine mingi ya bahati nasibu itakayokuja baadaye.
“Kampuni
yetu inao uzoefu wa muda mrefu kuendesha michezo ya Bahati Nasibu na
tutahahakikisha watanzania wananufaika na mchezo huu pia tutachangia
pato la taifa kwa njia ya kodi kupitia mchezo huu.Aliongeza kuwa
uchezeshaji wa mchezo utakuwa wa wazi kupitia vyombo vya habari na
mshindi atakuwa anatangazwa na kupatiwa fedha zake mara moja bila kuwepo
urasimu wa aina yoyote.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubatisha ya
Taifa,Abbas Tarimba aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hii kwa
kununua tiketi za kushiriki katika mchezo kutoka kwa mawakala
waliosambaa nchini kote ili waweze kujishindia zawadi ya mamilioni ya
fedha na kubadilisha maisha yao.
Tarimba
aliwataka wananchi wasiwe na hofu ya kushiriki kwenye mchezo kwa kuwa
unafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali
“Wananchi wasiwe na wasiwasi kushiriki kwenye mchezo huu kwa kuwa fedha
zao na kanuni za uendeshaji wa mchezo vinasimamiwa na serikali.
Alisema
ujio wa mchezo huu nchini mbali na kuwanufaisha washindi binafsi
utachangia kupanue wigo wa ajira kwa Watanzania wengi watakaosimamia
zoezi la ukatishaji tiketi katika vituo zaidi 20,000 vitakavyofunguliwa
Nchi nzima.
Tiketi
za mchezo huu zimeanza kuuzwa nchi nzima na wakati wa uzinduzi wa
huduma za kampuni mkoani Dodoma wananchi wengi walijitokeza kununua
tiketi za kushiriki na walishauri mtandao wa kuuza tiketi ufanyike
kupitia hata kwenye simu za mkononi ili kuwawezesha wananchi wengi
kushiriki kununua tiketi ambayo kila moja inauzwa shilingi 500/-
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni