SERIKALI KUMLINDA MKULIMA KWA KUANZISHA VITUO VYA UNUNUZI WA MAZAO.
Wakala wa Vipimo kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakusudia kuanzisha vituo
maalum vya ununuzi wa mazao ya wakulima (buying centres) katika
vitongoji nchi nzima ili kuondoa unyonyaji na ukandamizaji unaofanwa na
wachuuzi wa mazao ya wakulima.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi aliyetaka
kujua ni lini Serikali itasimamia sheria kuondoa unyonyaji unaofanywa na
wachuuzi wakati wa kununua mazao ya wakulima.
Alisema kuwa katika kutekeza
hayo hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kusafirisha mazao ambayo
yamefungashwa kinyume kinyume cha Sheria ya vipimo na kuongeza kuwa
katika kusimamia jambo hilo vitaanzishwa vituo maalum vya ukaguzi bila
kusabaisha usumbufu katika ufanyaji biashara.
Mhe. Mwijage amewaagiza Maafisa
Ugani walioko vijijini watumike kusimamia matumizi ya vipimo rasmi
katika vituo hivyo na kutoa taarifa zote muhimu kwa Wakala wa Vipimo.
Aidha ,alisema kuwa Serikali
imeamua kufanyia mapitio Sheria ya Vipimo sura 340 ili kuondokana na
unyonyaji na ukandamizaji unaofanywa na wachuuzi wa mazao ya wakulima.
Alisema kuwa Serikali imeamua
kufanyia mapitio ya Sheria hiyo ili kuweka mazingira mazuri kwa lengo la
kumlinda muuzaji kwa kuwadhibiti manunuzi wanaotumia njia za
udandanyifu wakati wanaponunua mazao ya wakulima.
Mhe. Mwijage alisema kuwa
katika kipindi kifupi kijacho Serikali itawalisha mabadiliko hayo
bungeni ili ifanyiwe marekebisho yanayostahili.
Aidha , Waziri huyo alisema
kuwa pamoja na marekebisho ya Sheria ya Vipimo yanatarajia kufanywa ,
Wakala wa Vipimo imewasilisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ndogo(by laws)
ili ziweze kuwaongoza wakulima na wafanyabiashara kufungasha mazao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni