ATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ATUNUKU VYEO KWA MAAFISA 327 WA JESHI LA MAGEREZA, CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA
Katibu
 Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira akiwa 
katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride Maalum 
lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili katika 
sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Maofisa wa Jeshi la Magereza, Chuo 
cha Magereza Kiwira kilichopo, Rungwe mkoani  Mbeya(kushoto) ni Kamishna
 Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Katibu
 Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Rwegasira akikagua moja ya
 Gadi ya Wanaume inayoundwa Gwaride rasmi la sherehe hizo.
Katibu
 Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira 
akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wanafunzi 
Wahitimu kwa niaba ya Wahitimu wote wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la 
Pili. Mwanafunzi huyo amefanya vizuri katika Mafunzo hayo.
Onesho
 Maalum la kujihami kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza katika namna 
ya kupambana na adui yeyote wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao
Kamishna
 Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akifurahia 
jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi(katikati). Kulia 
ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura. 
 
Askari
 Wanafunzi ambao wanaendelea na Mafunzo yao ya Awali wakifuatilia 
sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
Maafisa
 Wandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza 
wakiteta jambo mara baada ya kufungwa rasmi kwa Mafunzo ya Uongozi 
Daraja la Pili(kulia) ni ACP. Solomon Urio(katikati) ni ACP. Lazaro 
nyanga(kushoto) ni ACP. Ismail Mlawa(Picha zote na Lucas Mboje).
…………………………………………………………………………………….
Na; Lucas Mboje, Rungwe
JUMLA ya Askari 327 wa 
Jeshi la Magereza, kati yao wanaume 257 na wanawake 81 wametunukiwa  
cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza baada ya kuhitimu mafunzo ya 
Uongozi daraja la Pili kozi namba 1 katika Chuo cha Magereza Kiwira, 
Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Cheo hicho wametunukiwa
 na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali Projest 
Rwegasira katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika 
katika Viwanja vya Chuo hicho leo Mei 20, 2016.
Akizungumza katika 
sherehe hizo Meja Jenerali Rwegasira amesema Askari na Maafisa wa Jeshi 
la Magereza nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Haki za 
Binadamu na Utawala Bora kila wakati wanapotekeleza majukumu yao ya 
kazi.
Jenerali Rwegasira 
amesema Maafisa hao wahitimu wakazingatie elimu waliyopewa wakati wa 
mafunzo ili wakawe mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja 
na kuhamasisha na kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.
Aidha, amewaasa 
kutowatesa Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia 
kanuni na taratibu za uendeshaji wa magereza kwani Wafungwa ni Binadamu 
kama watu wengine ispokuwa tu wameikosea jamii.
“Tuzingatie falsafa ya 
kwamba mfungwa yupo gerezani kwa ajili ya kutumikia adhabu na si kwa 
kuongezewa adhani. Kwa kufanya hivyo, Serikali yetu itakuwa inazingatia 
Utawala wa Sheria na hivyo kuwa Taifa linalozingatia na kuheshimu Haki 
za Binadamu na Utawala Bora”. Alisisitiza Jenerali Rwegasira.
Akizungumza kabla ya 
kumkaribisha mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John 
Casmir Minja amesema kuwa changamoto nyingi ambazo kwa kiasi fulani 
zimeathili utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo ni pamoja na ufinyu wa 
bajeti, makazi duni ya maafisa na askari, uhaba wa vitendea kazi na 
uchakavu wa vyombo vya usafiri.
Kamishna Jenerali Minja
 ameongeza kuwa tayari Jeshi hilo limechukua hatua mbalimbali za kufanya
 maboresho kwa lengo la kufanya Jeshi la Magereza kuwa la kisasa katika 
kutekeleza majukumu yake kisayansi na kwa ufanisi unaotarajiwa.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni